Saturday, September 1, 2012

UCHAGUZI DRFA OKTOBA 14


KAMATI ya uchaguzi ya chama cha soka mkoa Dar es Salaam, DRFA leo kimetangaza utaratibu wa uchaguzi wa chama hicho unaotarajiwa kufanyika Oktoba 14 mwaka huu, baada ya kusimamishwa shirikisho la mpira wa miguu nchini TFF, kutokana na kasoro zilizokuwemo katika katiba yao.

Kamati imeamua kutangaza mapema fursa za wanaotaka kuwania uongozi ndani ya DRFA mapema kabla ya tarehe 3 tuliyopanga awali, ili kutoa wigo mpana zaidi ya wagombea. Septemba 10 itakuwa ni siku ambayo kamati ya uchaguzi itakaa na kuzipitia fomu zote na kuweka wazi kwenye mbao za matangazo majina ya waombaji uongozi DRFA.

Septemba 16 kutoa fursa ya pingamizi kwa waombaji uongozi. Mwisho wa kupokea pingamizi ni Septemba 20 saa 10 alasiri. Pingamizi ziwasilishwe kwa katibu wa kamati ya uchaguzi.

Hakutakuwa na ada katika kuweka pingamizi, bali pingamizi zizingatie matakwa ya ibara ya 11(2) ya kanuni za uchaguzi.

Ratiba hii inaonesha Septemba 26 ni fursa ya kukata rufaa iwapo maamuzi yaliyotolewa na kamati DRFA hayakurishishwa na mrufaa na hiyo itakwenda kwa kamati ya TFF.

Kampeni kwa wagombea zitaanza rasmi Oktoba 4, hadi13 ambapo Oktoba 14 itakuwa uchaguzi.  Pia katika kikao cha kamati ya uchaguzi ya DRFA kilichoketi Septemba 1, imetoa ufafanuzi  kuhusu waliochukua fomu awali kuwa watachukua tena, lakini hawatalipa ada ya kuchukua fomu.

Ada kwa nafasi ya Mwenyekiti, Makamu na Katibu ni Sh. 200,000 wakati nafasi nyingine zote ni Sh.100,000 na kuwa kipengele pekee kilichotakiwa marekebisho cha kiwango cha elimu kimerekebishwa na hakuna sehemu inayosema inayofanana na, bali elimu ya kidato cha nne.

 

 

 

No comments:

Post a Comment