Friday, August 31, 2012

TALENT MISS ILALA YACHENGUA

WAREMBO watano jana usiku, waliwafunika wenzao katika shindano dogo la kategoria ya kipaji Miss Ilala 2012 na kutangazwa kuingia tano bora ambapo mmojawapo atatangazwa mshindi katika fainali ya mashindano hayo,  Septemba 7 mwaka huu.

Katika shindano hilo lilofanyika katika ukumbi wa Nyumbani Lounge, kiukweli warembo hao walionesha uwezo mkubwa kwamba walijiandaa vilivyo katika kuhakikisha kila mmoja anampuki mwenzie, lakini mwishowe watano walitangazwa na majaji Khadija Mwanammbo na Matukio Chuma kuwa wamevuka hatua ya fainali.

Katika kinyanganyiro hicho mrembo Mary Chizi alikuwa kivutio zaidi kwa jinsi alivyoonesha umahiri wake wa wepesi wa kujvingirisha mwili huku Mectilda Martin akizoa ukumbi mzima kwa kurap na huku akiwa ameandana kwa kucheza hata mavazi yanayotumiwa na wasanii wa miondoko hiyo.

Magdalena Munisi haukuwa nyuma kabisa katika kumwigiza mwanamuziki nguli wa marekani, Ciara kwa umahiri wake wa kulitumia jukwaa, lakini kubwa kuliko pia kwa mrembo Amina Sangawe alibuni nguo kwa kutumia vipande viwili vya khanga ambapo aliliunganisha jukwaani kupitia pini nakumvika mmrembo mwenzie. Stella Moris kwa upande wake alionesha ukali kwa kuimba.

Mshindi wa taji hilo, atatajwa katika kilele cha shindano la Miss Ilala 2012 kwenye ukumbi huo huo, Septemba 7, mwaka huu. Shindano hilo lililoanza saa 3;00 usiku, lilipambwa na burudani ya bendi ya mapacha watatu na mastaa kibao wa bongo walikuwepo.

Warembo hao, wamekuwa wakijifua kwa takriban wiki nne sasa chini ya wakufunzi, Slyvia Mashuda ambaye ni Miss Tanzania namba mbili mwaka 2008 na Miss Ilala wa mwaka huo, na Neema Mbuya na Dickson Daudi wa THT katika shoo.

Miss Ilala, yenye rekodi ya kutoa warembo wanne waliotwaa taji la Miss Tanzania kuanzia mwaka 1999, (Hoyce Temu), 2000 (Jacquline Ntuyabaliwe aka K-Lyne), 2002 (Angela Damas Mutalimwa) na Salha Israel anayeshikilia taji hilo kwa sasa, imepania kuendeleza rekodi yake nzuri mwaka huu.
Miss Ilala inahusisha warembo kutoka vitongoji vya Dar City Center, Tabata na Ukonga na inadhaminiwa na City Sports Lounge, Redd's Premmium Cold, Uhuru One, Dodoma Wine, Nyumbani Lounge, gazeti la Jambo Leo,  100.5 Times FM, Redio ya watu 88.4 Cloud's FM.
 Mrembo Magdalena Munis akicheza kumwigiza mwanamuziki wa Kimarekani Ciara katika shindano hilo.
 Mrembo Mectilda Martin akionesha umahiri wake wa kurap jukwaani.
 Amina Sangawe (kulia) mara baada ya kumaliza gauni lake la ubunifu alilomvika mrembo mwenzie Elizaberth Perty alilotumia khanga kushikizia na pini
 Kama hawapo Nyumbani Lounge wakurugenzi wa City Sports Lounge, Juma Pinto(kushoto) na Benny Kisaka wakati wa shoo hiyo

No comments:

Post a Comment