Monday, August 27, 2012

YANGA YATUA BILA TWITE

MABINGWA wa soka Afrika Mashariki na Kati,Yanga  wametua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, dakika chache zilizopita bila mlinzi wake mpya aliye gumzo jijini, Mbuyu Twite.

Rwanda wametua wakitokea Rwanda walipokuwa kwa wiki moja kwa ziara ya mechi mbili za kirafiki na kufika Ikulu ya nchi hiyo kwa mwaliko wa Rais Paul Kagame, walicheza mchezo wa mwisho jana kwa kuwafunga Polisi ya nchini humo mabao 2-1, katika mchezo bngali
.
Yanga iliyomsajili Mbuyu Twite kutoka St Eloi Lupopo ya DRC, ingawa alikuwa anachezea APR. Katibu Mkuu wa Yanga, Celestine Mwesigwa amesema kuna mambo anakamilisha na atatua Dar es Salaam ndani ya saa 48 kuanzia leo.

“Tuna imani Jumamosi katika mechi yetu na Coastal Union Uwanja wa Taifa atakuwepo kutambulishwa rasmi,”alisema Mwesigwa. Kuhusu mpango wa Simba SC, kumfungulia kesi Polisi na kumvizia akitua tu nchini imkamate ikidai kuwatapeli dola za Kimarekani 30,000, Mwesigwa alisema; “Simba sio Polisi, na Yanga ni klabu ambayo inafanya mambo yake kwa utaratibu, kwa hivyo hatuna wasiwasi na hilo", alisema Mwesiga.

Mchezaji huyo awali inadaiwa  alisaini Simba na kupewa dola za Kimarekani 30,000 lakini baadaye akazirudisha kupitia viongozi wa APR na Lupopo, hatahivyo Simba walikataa kuzipokea.

Kutokana na sintofahamu hiyo, Simba SC waliamua kusajili beki Paschal Ochieng kutoka Kenya, ili kuziba pengo hilo, na hiyo baada ya kuonekana ngome yake ikipwaya katika mashindano ya kombe la Kagame. Katika mchezo wa awali Ijumaa, Yanga waliwachapa mabingwa wa zamani wa Afrika Mashariki na Kati, Rayon Sport mabao 2-0 kwenye Uwanja huo huo wa Amahoro.

Yanga iliyokwenda Rwanda na msafara wa watu 42, wakiwemo wachezaji 28, Maofisa watano wa benchi la Ufundi na viongozi wanane, baada ya kutua wataendelea na mazoezi keshokwenye Uwanja wa sekondari ya Loyola kujiandaa na Ligi Kuu ya Bara, itakayoanza Septemba 15 na Jumamosi itacheza na mabingwa wa Coastal Union ya Tanga kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment