Friday, August 24, 2012

HAPPY BIRTHDAY TO MY LOVELY SIZ GEE

May your birthday be filled with sunshine and smiles, laughter, love, and cheer, enjoy your day much love tupo pamoja
 

Ghymkhana wamtimua Ali Mafuruki

Wanachama wa klabu ya Gymkhana juzi walimuondoa Mwenyekiti wa klabu hiyo, Ali Mafuruki na viongozi wenzake na kuundwa kamati ya muda inayokaa madarakani hadi Septemba mwaka huu.

Katika mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa mikutano uliopo ndani ya viwanja Gymkhana Dar es Salaam, walifikia uamuzi wa kumuondoa Mafuruki kwa kuiendesha klabu hiyo kibabe na kuondoa taratibu nyingi ambazo zimekuwa kero kwa wanachama.

Hali iliyomfanya mmoja wa wanachama wa klabu hiyo, ambae ni Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), asiwe mbishi kujiondoa, kwani asiifanye Gymkhana kama Woorlworth ambayo ni moja ya kampuni anazomiliki Mafuruki.

Kufuatia uamuzi huo, wanachama hao wameteua kamati ya muda itakayoongozwa na Victor Kimesera na Makamu wake Erard Mutalemwa,  huku manahodha wa michezo yote wanaendelea na nyadhifa zao ambao ndio wanaounda kamati ya utendaji ya Ghymkhana.

Mkutano huo ulianza saa moja na nusu jana usiku huku kukiwa na polisi waliokuwa na lengo la kulinda usalama, lakini ulitawaliwa na jazba ya kumtaka Mafuruki ajiuzuru kwa madai kuiendesha klabu hiyo kinyume na taratibu na maamuzi mengi yamekuwa yake binafsi.

Hata hivyo, Mafuruki baada ya kuingia katika mkutano huo aliwaambia wanachama hao kuwa mkutano huo haukufuata taratibu hivyo maamuzi yoyote ambayo watayachukua yatakuwa yamekiuka katiba ya klabu hiyo na kususia kikao na kuondoka.

Wakati akiondoka wanachama hao walikuwa wakizomea, hali iliyofanya mmoja wa wadhamini wa klabu hiyo Jaji mstaafu, Stella Longway kuchukua jukumu la kuendesha kikao kwa mujibu wa katiba ya klabu hiyo na wanachama kufikia maamuzi ya kuwaondoa viongozi wote wa klabu hiyo.

Klabu hiyo mbali na Jaji Stella inawadhamini wengine wawili ambao ni G. Kilindu na Ritha Akena.Wadhamini hao wana mamlaka ya kufanya kazi hiyo kwa niaba ya wanachama wa klabu hiyo.

Kufuatia uamuzi huo, kamati hiyo ya muda inayoongozwa na Kimesera inatarajia kukutana hivi karibuni pamoja na mambo mengine ni kurudisha ada ya mgeni mwalikwa ‘Guest Fees” kutoka shilingi elfu 10 hadi elfu mbili kama zamani.

Hatua nyingine ni kurudisha utaratibu wa timu za Gymkhana kualika timu za nje kucheza mechi, hali ambayo uongozi wa Mafuruki ulipiga mafuruku kucheza mechi ndani ya viwanja hivyo au timu zinazokuja kulipiwa shilingi elfu 10 kwa kila mchezaji.

Mbali na Mafuruki kama Mwenyekiti, wengingine ni Makamu Mwenyekiti, Profesa Primo Carneiro,Katibu Nicholas Siwingwa, Mweka hazina, Nada Margwe, Mkuu wa wanachama, Santosh Gajjar, Mkuu wa viwanja, David Shambwe, Mkuu wa Bar, Alfred kinshwaga na Joseph Kusaga mkuu wa kitengo cha burudani.

Wengine ni manahodha michezo yao kwenye mabano ni Joseph Tango (Gofu),Inger Njiru (Tenisi),Chukkapalli Sriram (Kriketi),Ivan Tarimo (soka),Deepak Dosh (squashi) na Firoz Yusufunali (snooka)

Lakini wanachama hao wanakusudia kuwarudia wakuu wa vtengo vyote kasoro nafasi ya Mwenyekiti.
 

 

Yanga walipotinga Ikulu Rwanda

 Rais Paul Kagame wa Rwanda(kulia), akisalimiana na kusikiliza neno la mdhamini wa Yanga, Mama Fatuma Karume wakati rais huyo alipowakiribisha Ikulu, jijini Kigali jana.
 Rais Kagame wa Rwanda akisalimiana na kocha wa Yanga, Tom Saintfiet wakati rais huyo alipowakiribisha Ikulu, jijini Kigali jana.
 Mwenyekiti wa Yanga, Yusuph Mehmboob Manji(kulia), akimweleza jambo Rais Kagame katika Ikulu ya nchi hiyo jijini Kigali, juzi.
 Rais Kagame wa Rwanda(katikati) akishika kombe la Afrika Mashariki na Kati(Kagame Cup) sanjari na  kocha wa Yanga, Tom Saintfiet na nahodha Nadir Haroub Carnavaro wakati rais huyo alipowakiribisha Ikulu, jijini Kigali jana.
 Mdhamini wa Yanga, Mama Fatuma Karume(katikati) akimkabidhi jezi ya timu hiyo, Rais Kagame Ikulu Kigali, juzi. Kushoto ni Seif Ahmed 'Magari'wakati rais huyo alipowakiribisha Ikulu, jana.
Rais Kagame(kulia), akiteta jambo na Mwenyekiti wa Yanga, Yusuph Manji(Picha zote na Saleh Ally wa Champions.

Wednesday, August 22, 2012

NANCY SUMARI WITH HER NEW WEBSITE


"So idea hii niliipata baada ya kumpata Zuri, cause ninaenjoy sana maisha ya Umama na mtoto wangu anavyokua nazidi kujifunza vitu vingi zaidi.So i have decided kuanzisha a mommy blog ambapo nitakua nashare experience zangu na Mama wengine pamoja na kuwashirikisha wazazi kushare experience zao na watoto hao, pia na vingine vingi kama Mommy Fashion, Baby Fashion, Good Schools, Nutrition na vinginevyo, to be able to share and learn from others as well."... Says Nancy
visit the website http://mamazuri.com/

WATOTO NAO HAWAPO NYUMA


Tuesday, August 21, 2012

PEPLUM STYLE


Save the last for the best, jadore looking good in peplum

MY FAVORITE FASHION BLOGS OF THIS MONTH

Jadore
its all about fashion and she do it well i really enjoy her fashion spirit


she is good that's all i can say.

Monday, August 20, 2012

I Was Here (United Nations World Humanitarian Day Perform...


Musical powerhouse Beoncey is using her voice for a powerful message.
The 30-year-old Single Ladies songstress has debuted a new music video to benefit Sunday’s World Humanitarian Day.
Filmed at the UN General Assembly Hall in New York, the emotional performance features Bey belting out her hit, “I Was Here,” from her album 4 to raise awareness for global humanitarian work.
“We all see the headlines and we think what can I really do to help? World Humanitarian Day is an opportunity for all of us to work together to make a difference,” Beyonce says of her champaign with the United Nations. “This is our time to leave our mark on the world and show that we were here and we care.”

Tanzania chali Miss World

MWAKILISHI wa Tanzania katika mashindano ya urembo ya Dunia 2012, Lisa Jensen jana aliungana na warembo wengine 18 waliomtangulia kutoka Tanzania, kupigwa kumbo katika fainali hizo, baada ya mrembo wa China, Yu Wenxia  kutwaa taji hilo katika shindano lililofanyika Ordos Stadium Arena kaskazini mashariki ya jiji la kibiashara la Ordos.
Zilikuwa kelele zilizopitiliza baada ya mashabiki kushuhudia mrembo kutoka katika ardhi yao akitwaa taji hilo la 62, lililokuwa likishikiliwa na mrembo wa  Venezuela, Ivian Sarcosa ambaye jana alimvika taji malkia huyo mpya wa dunia katika mashindano yaliyoshirikisha nchi 116 kwa mara ya kwanza.
"Nikiwa mdogo nilisaidiwa na watu wengi sana, jambo ambalo ni fursa kwangu nami kufanya hivyo baada ya kutwaa taji hilo, ni bahati kubwa maishani mwangu", alisema Yu mbele ya waandishi wa habari akihojiwa kuhusu ushindi wake.
Sudan Kusini iliyoshiriki mashindano hayo kwa mara ya kwanza imefanya maajabu kwa kuingia hatua ya fainali ya mwisho kabisa ya saba bora. Katika 15 Kenya nayo ilitinga hatua hiyo ikiwa na  Sudani Kusini. Nchi za India,Mexico, Australia, Jamaica,China ,Wales, Uingereza, Brazil,Uhispania,Phillipines, Marekani, Uholanzi na Indonesia, nazo zilifika hatua hiyo.
Mbali ya China, ushindi wa pili ulikwenda kwa mrembo wales, Sophie Moulds wakati nafasi ya tatu ilikwenda kwa mrembo wa Australia, Jessica Kahawaty.  Taji hilo kwa mara ya kwanza mwaka 1951 lilitwaliwa na  Kiki Hakansson wa Sweden.Venezuela imewahi kutoa mrembo wa dunia mara sita wakati India na Uingereza zinafuatiwa kwa kutwaa mara tano.
Warembo wengine waliopata kushiriki miss World na miaka yao kwenye mabano ni pamoja na Aina Maeda(1994), Emilly Adolf(1995), Shose Sinare(1996), Saida Kessy(1997), Basila Mwanukuzi(1998), Hoyce Temu(1999), Jacquline Ntuyabaliwe 'K-Lyne'(2000),  Happiness Sosthnes Magese (2001), Angela Damas Mutalimwa(2002) na Sylvia Remmy Bahame(2003).
Wengine ni Faraja Kotta(2004), Nancy Sumari(2005), Wema Sepetu(2006), Richa Adhia(2007), Nasreem Karim(2008), Miriam Gerald(2009), Genevieve Emmanuel Mpangala(2010) na Salha Israel anayelishikilia taji hilo ambalo anatarajiwa kuanza kulivua Oktoba.
mwisho