Tuesday, August 28, 2012

NJE YA TANZANIA KUSHUDIA MISS ILALA

MASHABIKI wa urembo nchini na wale waliopo ughaibuni, kwa mara ya kwanza watalishuhudia moja shindanao la kumsaka mrembo wa Ilala 'stream live', kazi itakayofanywa kitaalam zaidi na kampuni ya Uhuru One.

Mbali ya mashabiki kupata faida hiyo ya kuoneshwa moja kwa moja kupitia mtandao, lakini faida kubwa kamati ya Miss Ilala imezingatia mchango wa wadhamini matangazo yao kuonekana nje ya mipaka ya jiji la Dar es Salaam na ughaibuni.

Ilala, ambao tunashikilia taji la Miss Tanzania kupitia Salha Israel, mwaka huu tumejiandaa vilivyo kuhakikisha taji hilo linaendelea kubaki katika manispaa yetu na ili katika kujiweka sawa na hilo, warembo wamekuwa wakijifua kwa takriban wiki nne sasa chini ya ukufunzi wa Slyvia Mashuda tayari kwa shindano hilo litakalofanyika Septemba 7 kwenye ukumbi wa nje wa Nyumbani Lounge.

Slyvia ni Miss Tanzania namba mbili mwaka 2008, akiwa Miss Ilala wa mwaka huo akishiriana na Neema Mbuya sanjari na Dickson Daudi wa THT katika shoo. Miss Ilala ambayo tumeshatoa warembo wanne waliotwaa taji la Miss Tanzania kuanzia mwaka 1999, (Hoyce Temu), 2000 (Jacquline Ntuyabaliwe aka K-Lyne), 20029( Angela Damas Mutalimwa) na  Vodacom Miss Tanzania, Salha Israel anayeshikilia taji hilo.

Warembo hao kutoka vitongoji vya Dar City Center, Tabata na Ukonga wamekuwa wakiendelea na mazoezi katika Club ya Nyumbani Lounge, iliyopo maeneo ya Namanga, Dar es Salaam. Washiriki hao ni pamoja na  Mary Chizi, Matilda Martin, Magdalena Munisi, Suzan Deodatus, Whitness Michael, Stella Moris na Elizaberth Pertty.

Warembo wengine ni Wilmina  Mvungi, Zawadi Mwambe, Rehema Said, Diana Simon, Amina Sangwe, Noela Michael na Phillios Lemi.

Mbali ya Uhuru One, Wadhamini wengine katika mashindano hayo ni pamoja na Dodoma Wine, City Sports Lounge, gazeti la Jambo Leo, Nyumbani Lounge, 100.5 Times FM, Redio ya watu 88.4 Cloud's FM na Redds Premmium Cold.


No comments:

Post a Comment