Thursday, August 30, 2012

KAPTENI GADNA G HABASH AANZISHA MASKANI TIMES FM

MTANGAZAJI Super Star bongo, Gadna G. Habash leo ametambulishwa rasmi kuhamia kituo cha redio cha 100.5 Times FM, baada ya kuwa nje ya kazi kwa takriban miaka miwili,  ambako alijikita zaidi katika kuanzisha na kuimarisha mgahawa wa Nyumbani Lounge.
Sauti yenye ubunifu wa hali ya juu katika uendeshaji kipindi cha mume wa mwanamuziki nyota Tanzania, Lady Jaydee 'aka' bint machozi sasa itakuwa ikisikika alichokibuni cha Maskani, kuanzia saa 10:00 jioni hadi saa1:00 usiku, muda ambao utakuwa sawia kabsia na kipindi alichokiasisi akiwa Cloud's FM cha Jahazi.
Kapteni G alikuwa akitangaza kipindi cha Jahazi Clouds kabla ya kubwaga manyanga Novemba mwaka 2010 katika kipindi ambacho redio hiyo ilipoteza mastaa wengi, wakiwemo Fina Mango, George Njogopa na Masoud Kipanya.  
Fina kwa sasa yupo Magic FM na Kipanya alimtangulia Gadna Times FM. Katika mkutano huo wa chakula cha mchana na wanahabari wa vyombo mbalimbali, mbali ya Gadna, Times pia iliwatambulisha wasanii Suzan Ngatwika 'Natasha na mwanae Monalisa kuwa wanaendesha kipindi kiitwacho Mama na Mwana.
 Gadna akizungumza na Waandishi wa Habari katika mgahawa wa City Sports Lounge mchana huu, katikati ya Jiji leo. Wengine kulia kwake ni Scholastica Mazula, Cliffor Ndimbo na Hadija Shaibu 'Dida'. Kulia ni Jabir Saleh.
Gadna kushoto akiwa na Schola na mtangazaji mwingine mpya wa Times, Natasha ambaye anatangaza kipindi cha Mama na Mwana.

No comments:

Post a Comment