Friday, July 20, 2012

RAIS KIKWETE ATUA ZANZIBAR KUFARIJI WALIOPATWA NA AJALI YA MELI

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji mmoja wa walionusurika katika ajali ya meli jana huko Chumbwe wakati Rais na Mama Salma Kikwete walipowatembelea kuwafariji na kuwapa pole katika hospitali kuu ya Mnazi Mmoja Jana.

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakitembelea Uwanja wa Maisara, Zanzibar, ambako ndiko miili ya marehemu
huletwa kwa utambuzi baada ya kuokolewa kwenye eneo la ajali  jana
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakitembelea Uwanja wa Maisara, Zanzibar, ambako ndiko miili ya marehemu
huletwa kwa utambuzi baada ya kuokolewa kwenye eneo la ajali  jana
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji mmoja wa walionusurika katika ajali ya meli jana huko Chumbwe wakati Rais na Mama Salma Kikwete walipowatembelea kuwafariji na kuwapa pole katika hospitali kuu ya Mnazi Mmoja jana.

 Rais Jakaya Kikwete na Mama Salma Kikwete wakimsikiliza mmoja wa walionusurika katika ajali ya meli jana Bw Kitwana Makama Haji ambaye kalazwa katika hospitali kuu ya Mnazi Mmoja jana

Rais Jakaya Kikwete na Mama Salma Kikwete wakimpa pole Bi Salome Abeli, mmoja wa walionusurika katika ajali hiyo ya meli. Yeye ni mfanyakazi wa Tanzania Automic Energy Commission akitokea Arusha kwenda Pemba Kikazi jana.

Thursday, July 19, 2012

Beyonce Debuts Blonde Braids and Carries Daughter Blue Ivy Carter in NYC

 Beyonce Knowles debuts new blonde braids in NYC with daughter Blue Ivy Carter on July 18, 2012Kigoma all Stars Concert in Kigoma

 wabunge on stage
makomando. 
 Umati.
 Umati.
 wabunge-halima na estherbulaya

 zitto kabwe welcomes
zittojukwani

TAARIFA YA MHESHIMIWA DKT. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, KUFUATIA AJALI YA KUZAMA KWA MELI YA MV SKAGIT ILIYOTOKEA TAREHE 18 JULAI, 2012, CHUMBE, ZANZIBARTHE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Jana tarehe 18 Julai, 2012, majira ya alasiri kumetokea ajali ya kuzama kwa meli ya MV SKAGIT katika eneo la Chumbe, Zanzibar.  Meli hiyo iliyokuwa ikitokea Dar es Salaam kueleka Zanzibar ilikuwa imebeba watu 290. Kati yao watu wazima 250, watoto 31 na wafanyakazi wa meli 9. 
Amiri Jeshi Mkuu, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete aliagiza vyombo vya ulinzi na usalama vya Serikali ya Muungano yaani JWTZ na  Polisi waanze kazi ya uokoaji mara moja.
          Kazi hiyo imefanywa kwa kushirikiana na vyombo vya usalama vya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na meli za makampuni binafsi.  Mpaka giza lilipokuwa limeingia na hivyo kazi ya uokoaji kusitishwa mpaka kutakapokucha tarehe 19 Julai, 2012, watu 136 walikuwa wameokolewa na maiti 31 zilikuwa zimepatikana.  Aidha, mali zilizokuwa kwenye meli hiyo hazikuweza kuokolewa. 
          Kufuatia ajali hiyo, Rais wa Jamhuri ya Muungano alizungumza na Dkt. Ali Mohamed Shein, Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.  Alimpa pole kwa ajali iliyotokea hasa kwa vifo na majeraha waliyopata Watanzania wenzetu na watu wasiokuwa raia wa Tanzania.  Alimuomba afikishe salamu za rambirambi kwa ndugu zetu waliopotelewa na jamaa zao na kuwapa pole waliopata majeraha na maumivu maungoni mwao. Rais wa Jamhuri ya Muungano alisema kuwa huu ni msiba wetu sote na kwamba majonzi yao ni majonzi yake na ya Watanzania wote.  Kwa ndugu zetu waliojeruhiwa tunawaombea kwa Mwenyezi Mungu awape ahueni na wapone haraka ili waweze kuendelea na shughuli zao za kujiletea maendeleo na kulijenga taifa letu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amempongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Ali Mohamed Shein na viongozi wote wa ngazi mbalimbali kwa uongozi wao thabiti tangu taarifa ya kutokea kwa ajali mpaka sasa.  Aidha, amewapongeza maafisa na askari wa vyombo vya ulinzi na usalama na wafanyakazi wa meli binafsi, kwa juhudi kubwa walizozifanya za uokoaji wa ndugu zetu waliopatwa na maafa haya makubwa na ya aina yake.  Amewataka waendeleze juhudi hizo leo na siku zijazo.
          Rais amewataka wananchi wawe na moyo wa subira na uvumilivu wakati kazi ya uokoaji inaendelea.  Kama ilivyofanyika katika ajali ya MV Spice Islander miezi 10 iliyopita, uchunguzi wa kina utafanyika kubaini chanzo cha ajali.
          Kutokana na ajali hiyo na msiba huu mkubwa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete, ametangaza maombolezo ya taifa ya siku tatu ambapo bendera zitapepea nusu mlingoti kuanzia leo, tarehe 19 Julai, 2012.
          Asanteni sana.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
19  Julai, 2012


Wednesday, July 18, 2012

PICHA MBALI MBALI ZA MAAFA YA KUZAMA KWA MELI ZANZIBAR

 Watalii na raia wa kigeni pia walikuwemo katika meli iliyozama hawa ni baadhi ya waliosalimikaMtoto aliyeokoka kutoka katika meli iliyozama


 Abiria aliyeokoka kutoka katika meli iliyozama Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Hamad Masoud Hamad akiwa katika hali ya huzuni Baada ya kushiriki katika uokoaji na kuwaona Majeruhiwaliookolewa katika Meli iliozama ya Star Gate wakiteremka hapo Bandarini Zanzibar

Boti ya KMKM ikiwa katika zoezi la kuokowa majeruhi
BREAKING NEWS: MELI YA MV KARAMA INASEMEKANA KUZAMA ENEO LA CHUMBE VISIWANI ZANZIBAR


Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana kupitia kwa mashuhuda Meli hiyo MV Karama ya Kampuni ya Seagal imezama baada ya kupinduka kichwa chini miguu juu katika eneo la Chumbe karibia na Visiwa vya Zanzibar.

Mashuhuda hao wanakisia kuwa takribani watu 200 walikuwa ndani ya meli hiyo hata hivyo watu kadhaa wameonekana wakiwa wanelea huku wakiwa wamevaa (Life Jackets) na kuwa boti zisizopungua 4 zimeshafika eneo la tukio kwa ajili ya kuwaokoa na Wahanga wa ajali hiyo wamepelekwa katika Hospitali ya Mnazi Mmoja

MASANJA MKANDAMIZAJI AWASHA MOTO IRINGA MJINI KATIKA UZINDUZI WA ALBAM YAKE YA HAKUNA JIPYA

Mungu alimtumia Emmanuel Mgaya (Masanja Mkandamizaji au Mchungaji Mtarajiwa) kuwakusanya watu katika Uwanja wa Samora mjini Iringa kushuhudia matendo makuu ya Mungu, ambapo msanii huyu alikuwa akizindua albamu yake ya "Hakuna Jipya" Masanja Mkandamizaji ni mkazi wa jijini Dar es Salaam ni mzawaliwa wa mkoa wa Iringa. Aliamua kufanya tamasha lake katika mkoa aliozaliwa.

Msanja Mkandamizaji aliwakusanya watu kutoka mikoa mbalimbali waliofika  kushuhudia uzinduzi huo. Wasanii wa filamu za kibongo kutoka Dar es Salaam walifika mahali pale kama. Odama, Ray, steve Nyerere, Davina, Chopa Mchopanga, Jacquline Wolper na wengine wengi walifika mahali pale.
Mbali na uimbaji masanja Mkandamizaji ni mchekeshaji katika kituo cha televisheni cha TBC1 "Orijino ze Commedy", kutokana na karama hiyo ya uchekeshaji amepata kibali cha kukubalika katika jamii.

Masanja kwa sasa anajiita "Mchungaji Mtarajiwa" anategemea kuwa mchungaji lakini anasema hajui itakuwa saa ngapi, siku gani na wapi ataanza huduma hiyo, ila anakuomba uzidi kumuombea.

Masanja akisindikizwa na waimbaji mbalimbali kutoka Iringa na mikoa mingine katika uwanja wa samora mjini Iringa

 Masanja Makadamizaji akikagua gwaride lake

 Waimbaji wakiwa pamoja na Masanja Mkandamizaji aliyeshika ubao kama alama ya bunduki

Hapa Mgeni Rasmi akiongea baada ya kuzindua waliokaa ni baadhi ya wabunge wa viti maalum na mkuu wa mkoa wa Iringa.

 JB wa Bongo Movie akiwa ameshika kibaza sauti pamoja na waigizaji wenzake

 JB toka bongo movie akitoa support kwa kununua DVD na Audio Cd

 Diwani wa kata ya kitanzini Manispaa ya Iringa Jesca hakuwa nyuma kutoa support kwa kununua DVD ya album ya HAKUNA JIPYA


Masanja Mkandamizaji na gwaride lake wakiingia jukwaani
 Naibu Waziri wa Elimu Milubo akizindua DVD na VCD

 Vicent Kigosi (Ray) akisalimia wakazi wa Iringa

 Jacquline Waolper akiwa na furaha kuona tamasha linaenda vizuri
Masanja Mkandamizaji akisoma risala