Friday, June 22, 2012

PUMZISHA NYWELE PIA BADILI MUONEKANO WAKO KWA KUSUKANYWELE ni miongoni vitu vinavyompa mwanamke ‘fahari’ Nywele huweza kubadilika muonekano wa mtu na akaonekana mrembo au akaonekana asiye na mvuto wowote.
Kupendeza au kuvutia kwa mwanamke kupitia nywele kutatokana na jinsi muhusika atakavyozitengeneza na kuzipendezesha nywele zake kwa staili tofauti.

Ipo mitindo mingi inayoweza kuzipendezesha nywele zako. Waweza kupendeza kwa kuzichana nywele zako vizuri, lakini waweza pia kusuka nywele zako na ukaonekana mrembo, mpya na unayevutia kila wakati.
Wanawake wengi wamezoea staili moja tu katika nywele zao. Wengi wanapenda kuchana nywele zao kwa mtindo wa kuzibana kwa kwenda nyuma kwa kuamini kuwa ndio staili inayowafaa. Lakini wanawake hao wanasahau au wanashindwa kuelewa kuwa hata wakisuka wanaweza kupendeza na kuwa warembo.

Ipo mitindo mingi ya kuzisuka nywele zako na ukapendeza sawasawa au zaidi ya mtu ambaye amezichana nywele zake. Waweza ukasuka nywele zako kwa kutumia rasta au hata bila rasta na ukapendeza vizuri kabisa.

Waweza pia kusuka nywele zako kwa kutumia rasta kwa mtindo wa kwenda nyuma au hata kwa rasta ndefu. Zipo staili nyingi ambazo waweza kutumia kusuka nywele zako na ukaonekana mpya kabisa.

Mwanamke anayesuka nywele mara nyingi huonekana mpya na halikadhalika huwa tofauti na ambaye amezoea kutengeneza nywele zake kwa mtindo mmoja wakati wote.

Ni vizuri kuwa mbunifu, kwa kusuka nywele zako kwa staili mbalimbali ili uwe mrembo kila mara.

Kumbuka zipo faida nyingi za kusuka nywele, kwanza, kusuka nywele kutazisaidia nywele zako kupumzika na madawa hasa kwa wale wanaoweka dawa ili kuzinyoosha.

No comments:

Post a Comment