Saturday, June 23, 2012

AFRICAN PRINT IN FASHION







Stripes Collection 













 Office wear

 Nabaki Africaaaaa


Beyonce' & Alicia


 Lovely NoteBook











MAHAKAMA KUU YA TANZANIA IMETOA AMRI YA KUSITISHA MGOMO WA MADAKTARI


Kufuatia Tangazo la Chama cha Madaktari nchini (MAT) la kuanza mgomo siku ya Jumamosi tarehe 23 Juni, 2012, Mahakama Kuu ya Tanzania,Kitengo cha kazi,Dar es Salaam imetoa amri ya kusitisha mgomo huo mpaka hapo pande zote mbili yaani Serikali na Chama cha Madaktari Tanzania (MAT) yatakaposikilizwa na kutolewa uamuzi.

·        Amri hiyo ya Mahakama imetolewa kufuatia maombi namba 73 ya 2012 yaliyowasilishwa chini ya hati ya dharura na Mwanasheria Mkuu wa Serikali dhidi ya Chama cha Madaktari Tanzania (MAT).Sababu za msingi amabazo zimepelekea Mahakama kuu kutoa amri hiyo upande mmoja ni pamoja na;

·        Iwapo mgomo huo utatokea utakuwa na kuwa amri hii isipotolewa madhara yake ni makubwa isiyoweza kufidiwa kwa namna yoyote ile kama vile kupoteza maisha n.k



·         Wajibu maombi,ambao ni MAT, inaundwa na Madaktari ambao wapo katika Sekta ambayo inatoa huduma mahsusi (essential service sector), Aidha Chama cha Madaktari Tanzania kimetangaza mgomo bila kufuatia taratibu zilizoanishwa katika Kifungu cha 76(1 na 2) cha Sheria ya Kazi (Employment and Labour Relations Act No 6 ya 2004.

Masharti hayo ni

·        Kuzuia wafanyakazi walio katika Sekta Muhimu kugoma na kama wakigoma,

·        Kuwepona makubalianao ya pamoja ya kutoa huduma za msingi wakati mgomo ukiendelea.

Kwa misingi hii,Mahakama Kuu ya Tanzania, kwa Chama cha Madktari Nchini na wanachama wake kusitisha na kutoshiriki katika mgonmo huo.

DEIDRE LORENZ USO KWA USO NA YATIMA WA KITUO CHA YATIMA CHA UPENDO

Mcheza sinema maarufu wa Marekani Deidre Lorenz ambaye alitua mjini Moshi jana kushiriki kwenye mbio za kimataifa za Mt. Kilimanjaro Marathon leo alikaa na watoto wa kituo cha yatima cha Upendo kinachoendeshwa na masista wa shirika la Precious Blood mjini Moshi. Lorenz aliingia kwa kishindo katika Manispaa ya Moshi na kueleza juu ya nia yake ya kuitangaza Tanzania nchini Marekni kwa kutumia usanii wake wa filamu.

 
Deidre Lorenz anashiriki katika mashindano ya Mt. Kilimanjaro Marathon ambayo yanaanza kutimua vumbi tarehe 24 Jumapili kuanzia Moshi klabu hadi Rau madukani na kurudi. Mbio za Mt. Kilimanjaro Marathon zilianzishwa na Marie Frances kutoka katika mji wa Bethesda nchini Marekni mwaka 1991 baada ya kuombwa na balozi wa zamani wa Tanzania nchini Misri kuja Tanzania kuanzisha mbio za marathon.

 
Deidre Lorenz anawakilisha kikundi cha Actors Guild ambacho kina lengo la kukusanya pesa kwa ajili ya kutibu ugonjwa wa saratani. Katika ziara yake kwenye kituo cha watoto yatima cha Upendo Deidre aliwasomea watoto hao hadithi mbalimbali za watoto. Aidha, aliwapa zawadi za fangi za kuchora, vitabu, daftari, kalamu, chocolate na zawadi nyingine kemkem zinazowaelimisha watoto.

 
Lorenz ameshiriki pia katika mahojiano na waandishi mbalimbali wa habari mjini Moshi na kueleza kuhusu nia yake ya kuitembelea Tanzania mara kwa mara. Amesema kuwa wazazi wake hususan bibi yake alimwambia kuwa Tanzania ni nchi yenye wanawake wenye sura nzuri sana. Aidha marafiki zake wamemwambia kuwa aje yeye kwanza ili wao waje katika mbio zinazofuata.

Klabu ya Mt. Kilimanjaro Marathon 1991 inakusudia kuwatumia watu maarufu kuja Tanzania ili waweze kuutangaza utalii pamoja na mazingira ya kuwekeza. Klabu hii ina lengo la kuanzisha marathon nyingine tena ambayo itajumuisha mbio na michezo mingine ya uwanjani.

 
Tutakuwa na wiki nzima ya mashindanio ya uwanjani na siku ya saba tutafanya mbio za marathon” alisema Rais wa Klabu hiyo Onesmo Ngowi alipokuwa anazungumza na waandishi wa bahari hapa Moshi. Ngowi alieleza kuwa ni muhimu Moshi/Tanzania ikawa na mashindano ya michezo mingi itakayowavutia watalii na wawekezaji wengi kuja Tanzania.

Akielezea kuhusu mikakati ya klabu yake kuendeleza mchezo wa riadha Ngowi ambaye pia ni Rais wa IBF/USBA katika bara la Afrika, Mashariki ya kati na Ghuba ya Uajemi alisema kuwa wameweka mikakati mingi itakayoifanya mji wa Moshi kuwa kitovu cha utalii katika mkoa wa Kilimanjaro.
Hizi mbio ni sehemu tu ya mikakati ya kuendeleza michezo katika mkoa huu ambao miaka ya sabini ulikuwa unaongoza kwa michezo katika nchi hii. “Tutashirikiana na mashirikisho ya michezo ya ndani na nje kuinua viwango vya wanamichezo wetu” alisema Ngowi ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Michezo katika mkoa wa Kilimanjaro. Alisema kuwa wameandaa mikakati mingi na kumalizia kuwa Tanzania ni yetu sote kwa hiyo tuna jukumu la kuchangia katika maendeleo yake.

 
Deidre Lorenz atakimbia mbio za Mt. Kilimanjaro Marathon jumapili ijayo na ataondoka usiku wa jumapili kurudi nyumbani kwake New York jiji linajulikana kama “The Big Apple” na Financial Capital of the World (Jiji la Fedha Duniani)

 

Friday, June 22, 2012

PUMZISHA NYWELE PIA BADILI MUONEKANO WAKO KWA KUSUKA



NYWELE ni miongoni vitu vinavyompa mwanamke ‘fahari’ Nywele huweza kubadilika muonekano wa mtu na akaonekana mrembo au akaonekana asiye na mvuto wowote.
Kupendeza au kuvutia kwa mwanamke kupitia nywele kutatokana na jinsi muhusika atakavyozitengeneza na kuzipendezesha nywele zake kwa staili tofauti.

Ipo mitindo mingi inayoweza kuzipendezesha nywele zako. Waweza kupendeza kwa kuzichana nywele zako vizuri, lakini waweza pia kusuka nywele zako na ukaonekana mrembo, mpya na unayevutia kila wakati.
Wanawake wengi wamezoea staili moja tu katika nywele zao. Wengi wanapenda kuchana nywele zao kwa mtindo wa kuzibana kwa kwenda nyuma kwa kuamini kuwa ndio staili inayowafaa. Lakini wanawake hao wanasahau au wanashindwa kuelewa kuwa hata wakisuka wanaweza kupendeza na kuwa warembo.

Ipo mitindo mingi ya kuzisuka nywele zako na ukapendeza sawasawa au zaidi ya mtu ambaye amezichana nywele zake. Waweza ukasuka nywele zako kwa kutumia rasta au hata bila rasta na ukapendeza vizuri kabisa.

Waweza pia kusuka nywele zako kwa kutumia rasta kwa mtindo wa kwenda nyuma au hata kwa rasta ndefu. Zipo staili nyingi ambazo waweza kutumia kusuka nywele zako na ukaonekana mpya kabisa.

Mwanamke anayesuka nywele mara nyingi huonekana mpya na halikadhalika huwa tofauti na ambaye amezoea kutengeneza nywele zake kwa mtindo mmoja wakati wote.

Ni vizuri kuwa mbunifu, kwa kusuka nywele zako kwa staili mbalimbali ili uwe mrembo kila mara.

Kumbuka zipo faida nyingi za kusuka nywele, kwanza, kusuka nywele kutazisaidia nywele zako kupumzika na madawa hasa kwa wale wanaoweka dawa ili kuzinyoosha.

MGOMO WA MADAKTARI KUANZA KESHO RASMI TANZANIA NZIMA


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda

SASA ni dhahiri kwamba mgomo wa madaktari nchi nzima haukwepeki kutokana na Serikali kukwepa kufanya mazungumzo na Chama cha Madaktari nchini (MAT) na badala yake kukimbilia mahakamani ikitaka kupigwa marufuku mgomo wa madaktari uliopangwa kuanza nchini kote kesho.

Hatua hiyo ya Serikali ambayo sisi tunadhani siyo ya busara, ilithibitishwa jana bungeni na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda wakati akijibu maswali ya papo kwa papo kutoka kwa wabunge. Kwa mshangao mkubwa wa wabunge wengi, Waziri Mkuu alisema suala la madai ya madaktari halizungumziki tena kutokana na MAT kuendelea kushikilia msimamo wake wa awali wa madaktari kupandishiwa mishahara na posho mbalimbali kwa viwango ambavyo Serikali haina uwezo wa kuvilipa.

Msimamo huo mkali wa Serikali umekifanya chama hicho cha madaktari kujibu mapigo kwa kutangaza jana kwamba kitaendesha mgomo wa madaktari usiokuwa na ukomo na kwamba kesho utafanyika mkutano jijini Dar es Salaam kuweka mikakati ya namna ya kuendesha mgomo huo. Mgogoro huo kati ya MAT na Serikali unaashiria kiama kikubwa hasa kwa wananchi wengi kutokana na kipato chao kuwa cha chini, hivyo kutoweza kumudu gharama za matibabu zinazotozwa katika hospitali binafsi.

Hakuna aliyemtazamia Waziri Mkuu kutoa kauli hiyo ambayo kwa tafsiri yoyote ile inaashiria shari, hasa baada ya Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Husein Mwinyi kuonyesha dhamira ya Serikali ya kutaka kushughulikia madai ya madaktari kwa njia ya majadiliano kwa kusema mapema wiki hii kuwa, Serikali ingekutana nao kujadili na kufikia mwafaka juu ya madai yao, huku akiwasihi madaktari kutofanya mgomo. Kauli hiyo ya Waziri Mkuu ambayo haikutegemewa bila shaka ndiyo imepandisha joto la mgogoro huo, huku hofu ya kufanyika kwa mgomo huo ikitanda nchi nzima.

Hali hiyo ya sintofahamu inakuja muda mfupi tangu nchi iliposhuhudia mgomo mkubwa wa wanataaluma hao mapema mwaka huu, mgomo uliosababisha mateso makubwa ambapo wagonjwa nchi nzima walilia na kusaga meno. Kishindo cha mgomo huo kiliitikisa nchi na kulilazimisha Bunge kuingilia kati na kuzirudisha pande hizo mbili kinzani katika meza ya mazungumzo. Tumeambiwa kuwa, katika kujaribu kuepusha maafa katika mgogoro unaoendelea hivi sasa, Bunge kupitia Kamati ya Huduma za Jamii, limeitaka Serikali kuchukua hatua za kuzuia mgomo wa wanataaluma hao kabla haujaanza.

Jambo linalojitokeza katika mgogoro huo usioisha ni kwamba pande zote mbili haziaminiani. Madaktari wanasema Serikali haina nia ya dhati na kwamba inashughulikia suala hilo kisiasa, huku Serikali nayo ikihisi kwamba kuna msukumo wa kisiasa katika madai hayo ya madaktari. Ndiyo maana mazungumzo kati ya pande hizo mbili yamekuwa yakisuasua na kuvunjika mara kwa mara. Na pengine ndiyo maana Serikali imekuwa haitekelezi ahadi ambazo imekuwa ikitoa kwa madaktari hao na kuamua kukaa kimya.

Tulionya mara kadhaa huko nyuma kupitia safu hii kwamba mwafaka na maridhiano hayawezi kupatikana katika mazingira kama hayo ya kutoaminiana. Tulishauri kwamba katika mazingira hayo, lazima wapatikane wapatanishi wanaokubalika na kuaminiwa na pande zote zilizo katika mgogoro huo. Tulikwenda mbele zaidi na kupendekeza majina ya watu mashuhuri na waadilifu tuliodhani wanaweza kusuluhisha mgogoro huo, huku tukishauri kwamba Serikali haiwezi kuwa msuluhishi wa mgogoro huo kwa sababu nayo ni sehemu ya tatizo.

Sasa nini kifanyike ili kuepusha mgomo ambao hapana shaka utaleta mateso na vifo kwa wananchi ambao hawana hatia? Tunashauri kwamba Serikali itulie, iondoe kesi mahakamani na kwa kushirikiana na viongozi wa madaktari ihakikishe wanapatikana wasuluhishi wanaokubalika kwa pande zote mbili. Tunawashauri madaktari nao wakubali ukweli kuwa, katika kutafuta maridhiano katika mgogoro kama huo, haiwezekani wapate kila kitu wanachokitaka. Ukweli ni kwamba baadhi ya madai yao hayatekelezeki, hivyo watatakiwa kulegeza misimamo yao na ndipo wasuluhishi wataweza kutoa maamuzi yatakayoridhiwa na pande zote mbili. 

TIMU 20 KUCHEZA LIGI DARAJA LA KWANZA (TFF)



 
TIMU 20 KUCHEZA LIGI DARAJA LA KWANZA
Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imeridhia mapendekezo ya Kamati ya Mashindano ya kutaka Ligi Daraja la Kwanza (FDL) kuwa na timu 20 badala ya 18 za sasa.
 
Lengo la mabadiliko hayo ni Ligi ya Taifa (NL) kuchezwa kwa kanda, hivyo msimu huu timu mbili zaidi (ukiondoa tatu ambazo zimeshapanda kutoka NL) zitaongezwa ili kufikisha idadi ya timu 20 katika FDL.

 
Timu ambazo zimepanda kutoka NL iliyochezwa katika vituo vitatu ni; Kanembwa JKT ya Kigoma iliyoongoza Kituo cha Kigoma, Ndanda SC ya Mtwara iliyoibuka kinara Kituo cha Mtwara na Polisi Mara iliyokamata usukani katika Kituo cha Musoma.
Kamati ya Utendaji pia imepitisha mapendekezo ya kuchezwa play off ili kupata timu mbili zaidi za kucheza FDL msimu huu. Timu zitakazocheza play off katika utaratibu utakaotangazwa baadaye na Kamati ya Mashindano ni tatu zilizoshuka kutoka FDL na tatu nyingine zilizoshika nafasi za pili katika NL kutoka vituo vya Kigoma, Mtwara na Musoma.

 
Timu tatu zilizoshuka FDL ni AFC ya Arusha, Samaria ya Singida na Temeke United ya Dar es Salaam wakati zilizoshika nafasi za pili katika NL na vituo vyao kwenye mabano ni Kurugenzi ya Iringa (Mtwara), Mwadui ya Shinyanga (Kigoma) na Tessema ya Dar es Salaam (Musoma).

 
Hata hivyo, timu zitakazoshuka kutoka Ligi Kuu bado zitaendelea kuwa tatu kama ilivyo kwa zitakazopandwa.
AWAMU YA KWANZA USAJILI MWISHO AGOSTI 10
Kipindi cha kwanza cha usajili wa wachezaji kwa ajili ya msimu wa 2012/2013 kitamalizika Agosti 10 mwaka huu kulingana na kalenda ya Matukio ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ya 2012/2013.
Uhamisho wa wachezaji unafanyika kuanzia Juni 15 hadi Julai 30 mwaka huu wakati kipindi cha kuacha wachezaji (sio wa Ligi Kuu. Wachezaji wa Ligi Kuu wanacheza kwa mikataba) ni kuanzia Juni 15- 30 mwaka huu.

 
Kwa klabu za Ligi Kuu kutangaza wachezaji watakaositishiwa mikataba yao ni kuanzia Juni 15-30 mwaka huu na usajili wa wachezaji unafanyika kuanzia Juni 15 hadi Agosti 10 mwaka huu.

Tunasisitiza kipindi cha usajili kiheshimiwe na mikoa yote kwa sababu usajili huo huo ndiyo utakaotumika katika michuano ya Kombe la FA. Kwa maana nyingine hakutakuwa na kipindi kingine cha usajili wa wachezaji kwa klabu zote nchini hadi hapo litakapofunguliwa dirisha dogo.

 
Mechi ya kufungua msimu ya Ngao ya Jamii (Community Shield) kati ya mabingwa wa Ligi Kuu, timu ya Simba na makamu bingwa Azam itachezwa Agosti 25 mwaka huu wakati Ligi Kuu itaanza Septemba Mosi mwaka huu, na Ligi Daraja la Kwanza (FDL) yenyewe itaanza Septemba 15 mwaka huu.

 
Ratiba ya Ligi Kuu itatolewa Julai 23 mwaka huu.
MISRI YAOMBA KUIKABILI NGORONGORO HEROES
Chama cha Mpira wa Miguu Misri (EFA) kimeomba mechi mbili za kirafiki kwa timu yao ya vijana na timu ya vijana wenye umri chini ya miaka 20 ya Tanzania (Ngorongoro Heroes).

 
EFA imeomba mechi hizo zichezwe Julai 3 na Julai 5 mwaka huu kwa masharti maalumu. Ikiwa zitachezwa Misri, mwenyeji (EFA) atagharamia Ngorongoro Heroes kwa malazi, chakula, usafiri wa ndani na sehemu ya kufanyia mazoezi.
Ikiwa mechi hizo zitachezwa Dar es Salaam, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) litaigharamia timu ya Misri kwa malazi, chakula, usafiri wa ndani na sehemu ya mazoezi. Hivyo kila timu itajigharamia kwa usafiri wa ndege na posho kwa timu yake.

 
Sekretarieti ya TFF inafanya uchambuzi wa gharama ili kujua ipi ni nafuu kabla ya kufanya uamuzi wa wapi mechi hizo zichezwe.

 
Ngorongoro Heroes imeingia raundi ya pili ya michuano ya Afrika ambayo fainali zake zitafanyika mwakani nchini Algeria baada ya kuitoa Sudan katika raundi ya kwanza.
Itacheza mechi ya kwanza ya raundi ya pili Julai 28 mwaka huu jijini Dar es Salaam wakati ya marudiano itakuwa Agosti 11 mwaka huu nchini Nigeria.
 

RAIS AREJEA TOKA DODOMA LEO

 Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akipokewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Saidi Mecky Sadik leo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere akitokea Dodoma katika ziara ya kikazi

MKUTANO MKUU WA DHARURA TWFA JUNI 23


MKUTANO MKUU WA DHARURA TWFA JUNI 23

Mkutano Mkuu wa Dharura wa Chama cha Mpira wa Miguu wa Wanawake Tanzania (TWFA) utafanyika Juni 23 mwaka huu kwenye ukumbi wa Msimbazi Centre, Dar es Salaam kuanzia saa 2.00 asubuhi.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa TWFA, Lina Kessy, ajenda kuu katika mkutano huo ni marekebisho ya Katiba ya chama hicho yanayotokana na maelekezo ya Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) juu ya marekebisho kwenye katiba za wanachama wake ambazo zina upungufu.

Tayari mapendekezo ya marekebisho hayo kulingana na mwongozo wa TFF yalishapitiwa na Kamati ya Utendaji ya TWFA.

Mbali ya Kamati ya Utendaji, wajumbe wengine wa mkutano huo ni Mwenyekiti, Katibu na mjumbe wa Mkutano Mkuu kutokana vyama vya mpira wa miguu wa wanawake vya mikoa ya Tanzania Bara.

Wajumbe watafikia kwenye hosteli ya Msimbazi Centre ambapo wanatakiwa kuripoti siku moja kabla ya mkutano huo.

Mgeni rasmi atakayefungua mkutano huo anatarajiwa kuwa Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Michezo katika Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Juliana Yasoda

RAMADHANI SHAURI AONESHWA MKANDA WA UBINGWA WA IBF AFRICA


Bondia Ramadhan Shauri akiwa ameushika Mkanda wa I.B.F Africaalipooneshwa kwa waandishi wa habari Dar es salaam jana. Mkanda huo atauwania pamoja na Sande Kizito wa Uganda, Diamond Jubilee Idd Pili. Kushoto ni Makamu wa Rais wa Kamisheni ya Ngumi za kulipwa Tanzania (TPBC) Madaraka Nyerere na Promota wa mpambano huo, Mkurugenzi wa Kitwe General Traders, Lucas Rutainirwa

Ramadhani Shauri akiwa na mkanda wa ubingwa wa IBF Africa

Thursday, June 21, 2012

MCHEZA SINEMA WA MAREKANI DEIDRE LORENZO ATUA MJINI MOSHI NA SHAUKU KUBWA YAKUONA KAMA KWELI MLIMA KILIMANJARO UKO TANZANIA

Deider Lorenz na Rais wa IBF-USBA

Mcheza sinema toka Marekani Deidre Lorenz amewasili mjini Moshi tayari kushiriki kwenye mbio za Mt. Kilimanjaro Marathon zitakazofanyika juni 24. Lorenz amwasili leo na ndege ya Ethiopian Airlines ambao ndio wafadhali wa mbio za Mt. Kilimanjaro Marathon zinazofanyika jumapili ya mwisho ya mwezi wa sita kila mwaka. 


Ujio wa Lorenz ambaye amecheza sinema nyingi zikiwamo Santorini Bule, Perfect Strangers, The Big Fight umeleta msisimko mkubwa katika mji huu mkuu wa Kilimanjaro. Ujio wake umefuatia matayarisho ya muda mrefu ambayo yanaendana na hadhi yake. 

Akizungumza na waandishi wa habari waliofika kumshuhudia mcheza sinema huyu, Lorenz alisema kuwa ameisikia kuwa mlima wa Kilimanjaro uko Kenya kwa kwa muda mrefu na ana furaha kubwa sana ya kufika ili kushughudia kuwa mlima huu maarufu duniani uko Tanzania. “Nimekuwa nautangaza sana ujio wangu kwenye blog na tovuti yangu, wapenzi wangu pamoja na watu wengi wanangojea kurudi kwangu nikawaambie niliyoyashughudia” alisema Deidre Lorenz ambaye ameshawahi kuteuliwa zaidi ya mara tatu kwa tuzo za Oscar. Lorenz alisema kuwa kwa miaka mingi alifikiri kuwa mlima Kiliamnjaro uko Kenya kwa jinsi nchi hiyo jiraniminavyoutangaza nchini Marekani.
“Sasa nimeona mwenyewe kwa macho yangu kuwa kweli mlima (Kilimanjaro) huu maarufu duniani uko Tanzania na sio Kenya” alisema Deidre Lorenz ambaye anaishi kwenye jiji la New York City linalofahamika kama jiji la pesa (International Financial Capital) la kimataifa. Lorenz ameshukia katika hoteli ya Bristol Cottages iliyopo karibu na benki ya Standard Chattered mkabala na bustani ya Manispaa ya Uhuru Park. 

Mji wa Moshi na viunga vyake vinarindima kwa ujio wa watalii wengi kutoka Marekani ambao wamekuja kushiriki kwenye mbio hizi zilizojijengea umaarufu mkubwa kwa kuitangaza Tanzania nchini Marekani. Mbio za Mt. Kilimanjaro Marathon zilianzishwa na Marie Frances mwaka 1991 baada ya kuombwa na balozi wa zamania wa Tanzania nchini Misri. 

Mbio hizi zimejijengea umaarufu mkubwa na zimeshawahi kupata tuzo nyingi baadhi zikiwa zimetolewa na Wonders of the World Magazine lenye wasomaji zaidi ya milioni 5 likiwa limezipa nafasi ya 2 kama mbio zenye hadhi ya kukimbiwa duniani wakati jarida la Forbes la Marekani lenye wasomaji wengi duniani limeipa nafasi ya kwanza. Ndio maana Manispaa ya Moshi itampa barabara na kuiita “Marie Frances Boulevard”mwaka 2009. 

Mbio hizi hukimbiwa na watalii wa Warekani wanaokuja Tanzania kupanda mlima Kilimanjaro na kutembelea mbuga za wanyama. Mt. Kilimanjaro Marathon zinajulikana kama 7 continental races zikiwa zinakimbiwa katika mabara 7 ya dunia. 

Ratiba ya Deidre Lorenz inaonyesha kuwa kesho ijumaa atakitemnbelea kituo cha watoto yatima cha Upendo kinachoendeshwa na watawa wa Precious Blood. Lorenz atakaa na watoto hao na kuwasomea hadithi mbalimbali za watoto zilizoandikwa na Waltz Disney mwandishi maarufu wa karne ya ishirini wa Marekani. 

Siku ya jumamosi atatembelea hospitali ya KCMC ambapo atakutana na manesi ili kuwapa shavu kwa kazi yao nzuri wanayoifanyia jamii. Jioni ya jumamosi atahudhuria Pasta Party ambapo atapata nafasi ya kukutana na wakimbiaji wengine na kuchagua namba ya kukimbia kesho yake siku ya jumapili tarehe 24 juni.

MWANZILISHI WA MBIO ZA MT. KILIMANJARO MARATHON AMSIFU RAISI KIKWETE


Mwanzilishi wa mbio za Mt. Kilimanjaro Marathon Marie Frances mji wa Bethesda nchini Marekani amemsifu Rais Jakaya Mrisho Kikwete kama kiongozi anayependa nchi yake na anayeona mbali. Marie Frances ametoa sifa hizo hapa mjini Moshi wakati Rais Kikwete akikutana na viongozi wa Chama Cha Riadha Tanzania (AT) kupanga mikakati ya kufufua riadha nchini hivi karibuni.

Frances ambaye aliwahi kukutana na Rais Kikwete wakati wa ufunguzi wa jengo la Tanzania House katika jiji la Washington DC amesema kuwa ni nadra sana kuona kiongozi wa nchi akikutana na viongozi wa chama cha mchezo wowote kuzungumzia maendeleo yake. Hii ni miujiza hata katika nchi kama Marekani.

Marie Frances amemuelezea Rais Kikwete kama mtu wa haiba ya kipekee mwenye akili na maono ya kuiendeleza Tanzania kufikia malengo ya Umoja wa Mataifa ya Millenia. “Nilimpenda sana nilipokutana naye jijini Washington. Ni kiongozi mwenye haiba ya kipekee” alisema Frances ambaye aliombwa na balozi wa zamani wa Tanzania nchini Misri kuja kuanzisha mbio za marathon nchini Tanzania mwaka 1990.

Marie Frances ambaye alikuwa mkuzaji (producer) wa Miss Universe pamoja na vipindi vya television huko Hollywwod nchini Marekani alihamia nchini Misri mwaka 1984 kuafanya kazi ya ABC kama mwandishi wa bahari. Akiwa nchini Mirsi, Marie Frances alianzisha mbio za Pyramid Marathon pamoja na Miss Universe ambazo ziitangaza sana nchi ya Misri. Ni wakati wa matamasha haya balozi wa Tanzania nchini Misri wakati huo alipomwomba aje Tanzania kuanzisha mbio za marathon ili kuitangaza Tanzania.


Frances alikuja Tanzania mwaka 1990 na kutaka kuanzisha mbio za Mt. Meru Marathon lakini alipofika tu mjini Moshi alivutiwa sana na mlima Kilimanjaro na hivyo kuiamua kuanzisha mbio za “Mt. Kilimanjaro Marathon” mwaka 1991. Mbio hizi hukimbiwa kila jumapili ya mwisho ya mwezi wa sita na zitatimiza miaka 22 tarehe 24 Juni mwaka huu.

Mt. Kilimanjaro Marathon zimeshapewa tuzo mbalimbali kama mbio za kimataifa. Gazeti la Wonders of the World lenye wasomaji zadi ya million 5 limezipa nafasi ya 2 kama mbio nzuri za kushiriki. Wakati jarida la kimataifa la Forbes limezipa nafasi ya kwanza kama mbio nzuri za kukimbia! Marie Frances pia ameanza kuwapeleka wanariadha wa Tanzania kukimbia nchini Marekani kwa kuwasaidia fedha za Visa za Marekani pamoja na tiketi za ndege kama inavyoonyesha picha ambapo mkimbiaji Nelson Brighton anapewa pesa na Mkurugenzi wa manispaa ya Moshi Benadetta Kinabo kwenda nchi Marekani mwezi ujao kwa ufadhili wake.Kwa sasa mbio hizi hufadhiliwa na shirika la ndege la Ethiopia.

Ni katika juhudi zake za kuutangaza mlima Kilimanjatro ndipo Manispoaa ya Moshi ikaipa jina la Marie Frances Boulevard barabara ya zamani ya Bustani Ale.

Mt. Kilimajaro Marathon itaanzia Moshi Klabu tarehe 24 Juni saa kumi na mbili asubuhi ambapo mbio za kilometa 42, 21, 10 na 5 zitashindaniwa na watalii toka Marekani pamoja na wakimnbiaji toka Moshi na Arusha.
Wakimbiaji wanajiandikisha kwa wingi Bristol Cottages hotel iliyopo mkabala na benki ya Standard Chattered karibu na Kilimanjaro Hospital katika Manispaa ya Moshi.

LATEST ON BIG BROTHER STARGAME (Day 45)


After a traumatic four weeks marred by drama and violence, Big Brother organised a Therapist for the traumatised Upvillers. The Housemates spoke at length with the Therapist, during a private session conducted in the Upville lounge. In the last fourteen days, four Housemates have been disqualified from StarGame after their verbal arguments turned physical.
There has also been a lot of confusion in Upville since Maneta and Roki were disqualified regarding the Evictions on Sunday night as many of the Housemates were not sure whether Evictions would continue as planned or not. Big Brother then put the Housemates out of their misery and notified them that despite Maneta and Rookie’s disqualification, Evictions will go on as planned this Sunday.
Meanwhile, after saving Prezzo from the Eviction gallows, Goldie feels she may have made a mistake. On Monday, Prezzo, Maneta and Barbz made up the Nominations list, however, Goldie exercised her Head of House powers to save her boyfriend Prezzo and put Keitta on the chopping block instead. Goldie however broke down during one of her Diary Room sessions and revealed how gutted she is that she betrayed her friend, Barbz!
In the Downville Diary Room, things got heated when a fight broke out between sisters,Talia and Tamara.Tamara complained that she hasn't had any one on one time with her sister in a while.  Talia replied by saying that she is tired of living in her sister’s shadow and that she wants to be an individual and be able to interact freely with other Housemates.
Housemates were also busy with preparations for their task presentation on Thursday evening for which they wagered 100%. Big Brother commissioned housemates to pick a partner and pamper each other with beauty treatments including manicures, pedicures and facials.

Set to get the party started in the Big Brother House this weekend is the energetic, fun and super cool DJ Malick. The talented Malawian is the host of Gowelo Beats and Crush Grooves on Power 101. He will also be keeping the audience on their feet at the live Sunday Eviction Show while Ghanaian rapper and songwriter M.anifest will be performing on the night.
The 91 day reality super-series Big Brother StarGame, produced for M-Net’s AfricaMagic, is being screened live 24/7 on DStv channels 197 & 198.
 
Keegan

Goldie




 

Wednesday, June 20, 2012

DIAMOND AVUTA TOYOTA LANDCRUISER PRADO

Diamond akiwa na gari lake jipya aina ya Toyota Land Cruiser Prado. 

Ufanyaji kazi kwa bidii umemfikisha hapo alipo Diamond msanii wa bongo flavour mwenye kipaji kikubwa na aliekubalika na jamii, diamond ameonyesha mafanikio makubwa mwaka huu hasa alipo onekana kwenye nyumba ya Bigbrother Star game ni big stape  Africa nzima iliangalia alivyo performe ilikua ni big opportunity kujitanganza nje na ndani ya nchi.



Tuesday, June 19, 2012

WAASIRA AMSHAMBULIA ESTHER BULAYA NA KUMUITA MFWASI WA CHADEMA

MH. Stephen Waasira

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu), Stephen Wassira na Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Esther Bulaya, juzi walizozana katika kile kinachoonekana kuwa ni kuwania madaraka katika Jimbo la Bunda mkoani Mara, katika uchaguzi mkuu 2015.

Sakata hilo lilitokea nje ya ukumbi wa Bunge mara baada ya kuahirishwa kwa kikao juzi usiku, ambapo Wassira alimfuata Bulaya na kumhoji kwamba kwanini alitoa maneno ya kuipinga bajeti ya Serikali.

Wassira ambaye pia ni Mbunge wa Bunda (CCM)
Alimwambia Bulaya: “Mimi ndiye Mbunge wa Bunda, wewe huwezi kujifanya ndiye uliyetumwa na wananchi kuja kusema maneno ya uwongo hapa, eti unaipinga bajeti ya Serikali, ni nani aliyekutuma?”

Waziri huyo alikwenda mbali na kumwambia mbunge huyo kijana kwamba, “wewe tunakufahamu una pande mbili (upinzani na CCM) na kila siku unashirikiana na Halima Mdee (Kawe-Chadema), tunakujua kwamba uko CCM na Chadema.”

Kutokana na kauli hizo, Bulaya alijibu mapigo akimwambia Wassira kwamba yeye akiwa mbunge wa CCM ana wajibu wa kukikosoa chama chake na hakuwa mtu wa kwanza kukataa kuunga mkono bajeti hadi hapo marekebisho yatakapokuwa yamefanywa.

“Mimi nina haki ya kuzungumza ndani ya Bunge na kusema kile ninachokiamini kama mbunge, wala hakuna mtu wa kuniwekea mipaka. Halafu kama ni uhusiano na wabunge wengine mbona wabunge wengi tu wa CCM wanashirikiana na upinzani?” alihoji Bulaya.

Wakati hayo yakiendelea Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha na mbunge mwingine wa Viti Maalum (CCM), Rosemary Kirigini walikuwa wakishuhudia.

Nahodha alitumia dakika chache kumsihi Bulaya kutojibu mashambulizi ya Wassira.

MH.JOHN MNYIKA ATOA MSIMAMO WAKE JUU YA KAULI YAKE ILIOMFUKUZISHA BUNGENI LEO!!!


Nitatoa tamko la kina baadae kuhusu kilichotokea lakini kwa ufupi ubovu wa bajeti hii ni matokeo ya udhaifu wa Rais Kikwete, yeye ndiye aliyesaini Mpango wa Taifa wa miaka mitano kama Kiongozi Mkuu wa Nchi tena kwa wino mwekundu kama Amiri Jeshi Mkuu. Na yeye ndiye Mwenyekiti wa baraza la mawaziri, bajeti hii iliyoacha kuzingatia mpango wa Taifa imepita kwenye baraza alilloliongoza, pia kushindwa kutekelezwa kwa bajeti iliyopita ni matokeo pia ya udhaifu wa taasisi ya Urais.
Pia kwa mujibu wa Katiba Rais ndiye ambaye anapeleka bajeti bungeni, Waziri mwenye dhamana anapeleka tu kwa niaba. Rais amepewa mamlaka makubwa juu ya bajeti ibara ya 99 imeweka mipaka kuhusu mambo ambayo bunge lina mamlaka nayo huku ibara ya 90 inasema bunge likikataa bajeti rais ana mamlaka ya kuvunja bunge. Hivyo Rais Kikwete anapaswa kuagiza Waziri wa Fedha bajeti iondolewe irudi kwenye baraza la mawaziri ikafanyiwe marekebisho!

MH. John Mnyika akitoka Bungeni

 

BIG BROTHER: ZIMBABWE'S ROKI AND MANETA DISQUALIFIED


Another day, another fight, another disqualification. Zimbabwe is out of the Big Brother Africa StarGame after two of its contestants, Roki and Maneta, turned on each other after a disagreement.
The two Upville contestants had a disagreement that turned nasty after Roki poured water on Maneta and she in turn, poured bleach on his face.
Roki then called for help from fellow mates who quickly intervened to save the situation but he had already sustained injuries and tears rolling down his eyes.
Biggie was forced to cancel Keitta‘s diary room session and call Maneta into the diary room before deciding to send them packing for contravening the rule of violence which is punishable by expulsion.
Menata, who had been nominated for eviction, walked into the diary room saying "it's all over, it's all over" with her hands on her head.
The two housemates had been bickering all day and Big Brother had warned them that they needed to abide by the clearly stated house rules forbidding violence and provocation but they chose to disregard this instruction.
This is the second fight in upville in fortnight after DKB's infamous slap on Zainab and they were disqualified.
Roki and Maneta will be provided with psychological and medical treatment and counseling to assist them with conflict and anger management.

Monday, June 18, 2012

PIGO KWA WAANDISHI WA HABARI

Marehem Willy Edward Ogunde
Mhariri Mkuu wa gazeti la Jambo leo na Jarida la Jambo Brand
Amefariki dunia mjini Morogoro usiku wakuamkia jumapili , alipo kwenda kuhudhuria Mkutano wa sensa ulioandaliwa na ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), mwili wa marehem umesafirishwa kuja Dar na kuhifandhiwa katika hopitali ya taifa Muhimbili, wakisubiri taratibu nyingine zikifwata.

Mwili wa marehem Willy Edward Oginde ukifikiswa katika hospitali ya taifa Muhimbili

Sunday, June 17, 2012

DID KANYE WEST REALLY TWEET A NUDE PHOTO OF KIM OR A LOOK ALIKE?

 
Unlike Kim Kardashian who Instagrams matching sneakers and performance photos of her rapper boo Kanye West, ‘Ye decided to hop on Twitter and post a naked photo of a female who was implied to be the reality starlet. Though the tweet was later deleted, the famed K-dash sister became a trending topic

Kanye West says he didn’t post -or delete- any nude photo on his Twitter account, be it of girlfriend Kim Kardashian or porn star Amia Miley. In fact, he hadn’t been using Twitter during the alleged time frame when he supposedly posted the sexy pic

The picture posted on twitter could  it be Kim Or Porn star Amia Miley?.........

AY & MWANA FA NDANI YA BIGBROTHER HOUSE

AY ndani ya Bigbrother House Jumapili hii 17th June,Mwaka huu ni wa wanamziki na ma Dj kutoka Tanzania kuonyesha vipaji vyao ndani ya Bigbrother House.


AY & MWANA FA


Wazee wakazi

REDDS MISS TANZANIA 2012 LISA JENSEN

 Miss Tanzania Lisa Jensen (katikati) baada kuvishwa taji


 Tano bora

Washirki wote walioshiriki shindano hilo