MKUTANO MKUU
WA DHARURA TWFA JUNI 23
Mkutano
Mkuu wa Dharura wa Chama cha Mpira wa Miguu wa Wanawake Tanzania (TWFA)
utafanyika Juni 23 mwaka huu kwenye ukumbi wa Msimbazi Centre, Dar es Salaam kuanzia
saa 2.00 asubuhi.
Kwa
mujibu wa Mwenyekiti wa TWFA, Lina Kessy, ajenda kuu katika mkutano huo ni
marekebisho ya Katiba ya chama hicho yanayotokana na maelekezo ya Kamati ya
Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF) juu ya marekebisho kwenye katiba za wanachama wake ambazo zina upungufu.
Tayari
mapendekezo ya marekebisho hayo kulingana na mwongozo wa TFF yalishapitiwa na
Kamati ya Utendaji ya TWFA.
Mbali
ya Kamati ya Utendaji, wajumbe wengine wa mkutano huo ni Mwenyekiti, Katibu na
mjumbe wa Mkutano Mkuu kutokana vyama vya mpira wa miguu wa wanawake vya mikoa
ya Tanzania Bara.
Wajumbe
watafikia kwenye hosteli ya Msimbazi Centre ambapo wanatakiwa kuripoti siku
moja kabla ya mkutano huo.
Mgeni rasmi atakayefungua mkutano huo anatarajiwa kuwa Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Michezo katika Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Juliana Yasoda
No comments:
Post a Comment