Kufuatia Tangazo la Chama cha Madaktari nchini (MAT) la kuanza
mgomo siku ya Jumamosi tarehe 23 Juni, 2012, Mahakama Kuu ya Tanzania,Kitengo
cha kazi,Dar es Salaam imetoa amri ya kusitisha mgomo huo mpaka hapo pande zote
mbili yaani Serikali na Chama cha Madaktari Tanzania (MAT) yatakaposikilizwa na
kutolewa uamuzi.
·
Amri
hiyo ya Mahakama imetolewa kufuatia maombi namba 73 ya 2012 yaliyowasilishwa chini
ya hati ya dharura na Mwanasheria Mkuu wa Serikali dhidi ya Chama cha Madaktari
Tanzania (MAT).Sababu za msingi amabazo zimepelekea Mahakama kuu kutoa amri
hiyo upande mmoja ni pamoja na;
·
Iwapo
mgomo huo utatokea utakuwa na kuwa amri hii isipotolewa madhara yake ni makubwa
isiyoweza kufidiwa kwa namna yoyote ile kama vile kupoteza maisha n.k
·
Wajibu maombi,ambao ni MAT, inaundwa na
Madaktari ambao wapo katika Sekta ambayo inatoa huduma mahsusi (essential
service sector), Aidha Chama cha Madaktari Tanzania kimetangaza mgomo bila
kufuatia taratibu zilizoanishwa katika Kifungu cha 76(1 na 2) cha Sheria ya
Kazi (Employment and Labour Relations Act No 6 ya 2004.
Masharti hayo ni
·
Kuzuia
wafanyakazi walio katika Sekta Muhimu kugoma na kama wakigoma,
·
Kuwepona
makubalianao ya pamoja ya kutoa huduma za msingi wakati mgomo ukiendelea.
Kwa misingi hii,Mahakama Kuu ya
Tanzania, kwa Chama cha Madktari Nchini na wanachama wake kusitisha na
kutoshiriki katika mgonmo huo.
No comments:
Post a Comment