Mcheza
sinema maarufu wa Marekani Deidre Lorenz ambaye alitua mjini Moshi jana
kushiriki kwenye mbio za kimataifa za Mt. Kilimanjaro Marathon leo alikaa na
watoto wa kituo cha yatima cha Upendo kinachoendeshwa na masista wa shirika la
Precious Blood mjini Moshi. Lorenz aliingia kwa kishindo katika Manispaa ya
Moshi na kueleza juu ya nia yake ya kuitangaza Tanzania nchini Marekni kwa
kutumia usanii wake wa filamu.
Deidre Lorenz
anashiriki katika mashindano ya Mt. Kilimanjaro Marathon ambayo yanaanza kutimua
vumbi tarehe 24 Jumapili kuanzia Moshi klabu hadi Rau madukani na kurudi. Mbio
za Mt. Kilimanjaro Marathon zilianzishwa na Marie Frances kutoka katika mji wa
Bethesda nchini Marekni mwaka 1991 baada ya kuombwa na balozi wa zamani wa
Tanzania nchini Misri kuja Tanzania kuanzisha mbio za marathon.
Deidre Lorenz
anawakilisha kikundi cha Actors Guild ambacho kina lengo la kukusanya pesa kwa
ajili ya kutibu ugonjwa wa saratani. Katika ziara yake kwenye kituo cha watoto
yatima cha Upendo Deidre aliwasomea watoto hao hadithi mbalimbali za watoto.
Aidha, aliwapa zawadi za fangi za kuchora, vitabu, daftari, kalamu, chocolate na
zawadi nyingine kemkem zinazowaelimisha watoto.
Lorenz ameshiriki
pia katika mahojiano na waandishi mbalimbali wa habari mjini Moshi na kueleza
kuhusu nia yake ya kuitembelea Tanzania mara kwa mara. Amesema kuwa wazazi wake
hususan bibi yake alimwambia kuwa Tanzania ni nchi yenye wanawake wenye sura
nzuri sana. Aidha marafiki zake wamemwambia kuwa aje yeye kwanza ili wao waje
katika mbio zinazofuata.
Klabu ya Mt.
Kilimanjaro Marathon 1991 inakusudia kuwatumia watu maarufu kuja Tanzania ili
waweze kuutangaza utalii pamoja na mazingira ya kuwekeza. Klabu hii ina lengo la
kuanzisha marathon nyingine tena ambayo itajumuisha mbio na michezo mingine ya
uwanjani.
“Tutakuwa na wiki
nzima ya mashindanio ya uwanjani na siku ya saba tutafanya mbio za marathon”
alisema Rais wa Klabu hiyo Onesmo Ngowi alipokuwa anazungumza na waandishi wa
bahari hapa Moshi. Ngowi alieleza kuwa ni muhimu Moshi/Tanzania ikawa na
mashindano ya michezo mingi itakayowavutia watalii na wawekezaji wengi kuja
Tanzania.
Akielezea kuhusu
mikakati ya klabu yake kuendeleza mchezo wa riadha Ngowi ambaye pia ni Rais wa
IBF/USBA katika bara la Afrika, Mashariki ya kati na Ghuba ya Uajemi alisema
kuwa wameweka mikakati mingi itakayoifanya mji wa Moshi kuwa kitovu cha utalii
katika mkoa wa Kilimanjaro.
Hizi mbio ni sehemu
tu ya mikakati ya kuendeleza michezo katika mkoa huu ambao miaka ya sabini
ulikuwa unaongoza kwa michezo katika nchi hii. “Tutashirikiana na mashirikisho
ya michezo ya ndani na nje kuinua viwango vya wanamichezo wetu” alisema Ngowi
ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Michezo katika mkoa wa Kilimanjaro.
Alisema kuwa wameandaa mikakati mingi na kumalizia kuwa Tanzania ni yetu sote
kwa hiyo tuna jukumu la kuchangia katika maendeleo yake.
Deidre Lorenz
atakimbia mbio za Mt. Kilimanjaro Marathon jumapili ijayo na ataondoka usiku wa
jumapili kurudi nyumbani kwake New York jiji linajulikana kama “The Big Apple”
na Financial Capital of the World (Jiji la Fedha Duniani)
No comments:
Post a Comment