Thursday, July 26, 2012

Biggie’s Special Surprise!

 The remaining seven Big Brother StarGame Housemates received a pleasant surprise on Day 79 when Nigerian superstar 2Face paid them a visit in the afternoon and took them through the importance of the Thrive Garden. He emphasised the level of starvation in Africa and encouraged the Housemates to add their voice in the fight against poverty. "You are now celebrities so your voice is important," he said. As if that was not enough, 2Face then ushered the Housemates to the lounge where they received a message from the ONE Campaign founder Bono of U2 fame.







Wednesday, July 25, 2012

RAIS KIKWETE AONGOZA MAADHIMISH​O YA SIKU YA MASHUJAA KATIKA BUSTANI YA MNAZI MMOJA JANA

 Rais akiwasili Mnazi Mmoja

Wimbo wa Taifa










NIGERIA U20 YAWASILI KUIKABILI NGORONGORO HEROES

Timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 20 ya Nigeria (Flying Eagles) inatarajia kuwasili nchini leo (Julai 25 mwaka huu) saa 10 jioni kwa ndege ya RwandAir ikiwa na msafara wa watu 30 wakiwemo wachezaji 18.

Flying Eagles itapambana na Ngorongoro Heroes katika mechi ya kwanza ya raundi ya pili itakayofanyika Jumapili (Julai 29 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10 kamili jioni.

Mechi hiyo ya kuwania tiketi ya kucheza fainali za 18 za Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 20 zitakazochezwa mwakani nchini Algeria itachezeshwa na waamuzi kutoka Kenya wakati Kamishna ni Charles Masembe kutoka Uganda.

Flying Eagles inayofundishwa na kocha John Obuh, jana (Julai 24 mwaka huu) ilicheza mechi ya kirafiki na Rwanda (Young Amavubi) kwenye Uwanja wa Amahoro jijini Kigali. Nigeria ililala bao 1-0.

Msafara wa timu hiyo unaongozwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Nigeria (NFF), Chris Green. Baadhi ya wachezaji walioko katika kikosi cha Flying Eagles ni Chidi Osuchukwu, Alhaji Gero, Shehu Abdullahi, Aminu Umar, Aliyu Mohamed, Uche Agbo, Jonah Usman, Harrison Egbune, Hassan Abubakar na Yahya Adamu.

Viingilio katika mechi hiyo vitakuwa sh. 3,000 kwa viti vya rangi ya chungwa, bluu na kijani wakati VIP B na C itakuwa sh. 5,000. Kiingilio kwa VIP A itakuwa sh. 10,000.


              NUSU FAINALI KOMBE LA KAGAME
Nusu fainali zote mbili za kuwania Klabu bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kombe la Kagame) mwaka 2012 zinachezwa kesho Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kwa viingilio vya sh. 5,000, sh. 7,000, sh. 15,000 na sh. 20,000.

Azam na AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) zitacheza nusu fainali ya kwanza kuanzia saa 8 kamili mchana, na kufuatiwa na nusu fainali ya pili kati ya Yanga na APR ya Rwanda itakayoanza saa 10 kamili jioni.

Nisihusishwe na Matamshi na Makanusho wa Wabunge walokuwa Kigoma by zittokabwe

Katika gazeti la Mwananchi la tarehe 23 Julai 2012, kulikuwa na habari yenye kusomeka 'Wabunge wamsafishia Zitto njia ya Urais 2015'. Habari hii imeleta mjadala mara baada ya kutoka na kusomwa. Mjadala umekuzwa zaidi baada ya Wabunge ndugu Halima Mdee na ndugu Joshua Nassari kukanusha maneno waliyonukuliwa kuyasema. Napenda kusema masuala yafuatayo.

Moja, Waheshimiwa Wabunge Halima Mdee, Joshua Nassari, Kangi Lugola, Esther Bulaya, Deo Filikunjombe, Raya Ibrahim, Amina Mwidau na David Kafulila walihudhuria tamasha la vijana wa Kigoma All Stars kwa kualikwa na Mratibu wa kundi hilo Mwasiti Almasi.

Wabunge wengine walialikwa lakini hawakutokea wakiwemo Joseph Mbilinyi, David Silinde, Amos Makala, Vicky Kamata na Peter Serukamba. Wabunge hawa hawakualikwa na mimi bali nilisaidia 'logistics' tu. Lengo la kushauriana na Vijana wa Kigoma All Stars kuwaalika wabunge kutoka vyama mbalimbali lilikuwa ni kuonyesha umoja na mshikamano wa nchi bila kujali vyama vya siasa.

Wabunge wote walioalikwa waliambiwa hii ni shughuli ya muziki na wala sikufanya mazungumzo nao yeyote ya awali au kuwaambia au kukubaliana nini cha kuzungumza au hapana. Tamasha lilikuwa la muziki na halikuhusika kabisa na siasa. Ni bahati mbaya sana kuwa kuna matamshi ya kisiasa yalitamkwa katika shughuli ile.

Waheshimiwa wote walipewa nafasi ya kusalimia na wote walizungumza. Wabunge waliozungumza kwa muda mrefu kidogo ni ndugu Halima Mdee, Joshua Nassari, Deo Filikunjombe na Kangi Lugola.
Hotuba za Wabunge wote zilirekodiwa kwenye video neno kwa neno na video hizo zitawekwa wazi kwenye blogu yangu kama sehemu ya documentary ya tamasha lile la kihistoria.

Pili, sikuhusika kwa namna yeyote ile na kuandikwa kwa habari hii iliyozusha mjadala. Wala sikujua kama habari hii ingeandikwa maana katika ziara ile sikuita mwandishi hata mmoja maana nilitaka liwe tukio la Kigoma tu. Mimi kama mlezi wa KigomaAllStars na vijana wenyewe tulijikita katika 'shukrani Kigoma' kwa watu wa Kigoma.

Kama mwandishi kaandika ambayo wabunge hawa hawakuyasema basi itaonekana kwenye videos hizo. Wabunge wenyewe wanajua kwenye nafsi zao nini walisema Kigoma na kipi kiliwasukuma kusema walioyasema Kigoma.

Nisingependa kuhusishwa kwa njia yeyote ile na matamshi yao, habari iliyowanukuu na hata makanusho yao. Maana mwisho wa siku ukweli ndio utasimama.

Suala la Urais lisitupotezee muda kwani kuna mambo mengi sana ya kujadili kuhusu nchi yetu. Taharuki ambazo watu wanazipata masuala ya urais yanapotajwa zinashangaza sana.

Chama changu bado hakijatangaza rasmi mchakato wa kupata mgombea Urais. Hivi sasa chama hakina mgombea Urais mpaka hapo mchakato utakapotangazwa ambapo wanachama wataruhusiwa kuomba kupeperusha bendera ya chama. Mwanachama wa chama chetu atakaye kubalika na jamii na wajumbe wa mkutano wa uteuzi ndiye atakuwa mgombea wetu. Kwa sasa hayupo na hivyo tusipoteze muda kujadili jambo hili.

Mzee Thabiti Kombo alituachia usia tunapokuwa tunazungumza. Alisema 'weka akiba' sio akiba ya fedha, bali ya akiba ya maneno. Tuweke akiba ya maneno. Tusimalize yote.
zittokabwe | July 25, 2012

Tuesday, July 24, 2012

UBUNIFU WA KITENGE



i luv this one
 my best

CNN MultiChoic​e Africa Journalist Awards 2012 Winners

CNN African Journalist Awards Finalists 2012

AJALI YA BASI LA TONY SLEY YAUA RAIA WAWILI WA ZAMBIA NA MTANZANIA MMOJA IRINGA ,38 WAJERUHIWA

 Basi la Tony Sley ambalo limepata ajali usiku wa leo na kuua watu watatu na kujeruhi 38



 Majeruhi wa basi la Tony Sley Bi Agnesy Lukasi akiwa na mtoto wake Dina Lukasi (4) katika Hospital ya mkoa wa Iringa baada ya kufikishwa hapo wakitokea eneo la ajali mlima wa Kitonga
 Majeruhi Vedastus Benjamin (11) mkazi wa Tunduma akisubiri kupewa matibabu katika Hospitali ya mkoa wa Iringa
Dereva wa basi hilo akifikishwa hospitali 

Ajali mbaya ya basi ya Tony Sley yenye namba za usajili T 218 ACH lililokuwa likitokea Tunduma mkoani Mbeya kwenda jijini D’Salaamimeua watu watatu wakiwemo wawili raia ya Zambia na mmoja mtanzani huku watu 38 wakijeruhiwa .
Ajali hiyo imetokea katika eneo la kona za mlima wa kitonga kwenye barabara kuu ya Iringa –D’Salaam leo majira ya saa 12 za jioni baada ya dereva wa basi hilo kushindwa kulipita lori lilolokuwa mbele yake .
Wakizungumza na mtandao wa www.francisgodwin.blogspot.com majeruhi wa ajali hiyo waliolazwa katika hospitali ya wilaya ya Kilolo Ilula walisema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wao alisema Agnes Lukasi (30) .
Bi Agnesy alisema kuwa kwa upande wake alikuwa amekaa siti ya mbele na wakati dereva huyo akifanya uzembe huyo walikuwawakimshuhudia hata kujaribu kumuonya bila mafanikio .
Alisema kuwa katika basi hilo alikuwa na mtoto wake Dina Lukas (4) ambaye pia amejeruhiwa katika paji lake la uso .
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa Michael Kamhanda ambaye alifika eneo la tukio pamoja na mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Iringa aliuthibitishia mtandao huo kuwa jumla ya abiria 38 ndio waliojeruhiwa katika ajali hiyo.
Aliwataja baadhi ya majeruhi ambao majina yao yamepatikana na kulazwa katika hospital teuli ya mkoa wa Iringa kuwa ni pamoja na Boyd Simwings(43) , Violet Chambale(35),Zilombo Wake(38),Warmen Mambwe (33),Eugen Maluge(39), Mwamba Andrew (27) , Bright Mwalukanga (33) na John Lemba( 30) wote raia wa Zambia.
Wengine ni Martine Shombe( 29) mkazi wa Tunduma, Zainabu Amuri (32) mkazi wa D’Salaam , Efrain Mwampashi (31) mkazi wa Tunduma, Sebastian Mhaya(25) mkazi wa Tunduma, Vedastus Benjamin (11) mkazi wa Tunduma, Mrashi Handu (38) mkazi wa Igulusi, Juma Ramadhan (40) mkazi wa Tunduma, Twaribu Juhim (39) mkazi wa Arusha, Muka Muka (26) mkazi wa Tunduma, Edina Ramadhan (3) mkaziwa Tunduma na Benjamin Enock (33) mkazi wa Mbeya
Wengine ni Agness Lukas (30) mkazi wa Tunduma , Dina Lukas (4) mkazi wa Tunduma Beatrice Msakanti( 42) mkazi wa Zambia, Besa Shadrack (32) mkazi wa Zambia na Mary Mumba (48) mkazi wa Zambia pia.
Alisema majina ya majeruhi zaidi yatapatikana hivi karibuni baada ya majeruhi waliopo Hospital ya wilaya ya Kilolo Ilula kufika mjini Iringa .
Mbali ya majeruhi hao pia aliwataja waliopoteza maisha katika ajali hiyo kuwa ni Cla Pily (32) na Dany Kawina (43) wote wafanyabiashara raiawa Zambia pamoja na Abel Nelson (32) ambaye ni mtanzania.
Kamanda Kamhanda mbali ya kueleza masikitiko yake juu ya ajali hiyo bado aliwaonya madereva kuzingatia sheria za usalama barabarani na kuendesha kwa uangalifu wa hali ya juu na kuwa jeshi lake mkoani Iringa halitalala kuwabana madereva wazembe

Monday, July 23, 2012

WAZIRI WA MIUNDO MBINU ZANZIBAR AJIUZURU


Waziri wa Miundombinu Zanzibar, Mh.Hamad Masoud Hamad (CUF)amejiuzuru kufuatia ajali ya boti ya Skagit.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Mohamed Shein ameridhia kujiuzuru kwa waziri huyo na amemteua Mh. Rashid Seif Suleiman (CUF)kushika wadhifa huo.
Makamu wa Pili wa Rais ,Balozi Seif Iddi amesema uamuzi wa kujiuzuru wa Mh. Hamad ni uamuzi wake binafsi.

Sunday, July 22, 2012

“UTALII WA MICHEZO” - IBF YAKUSUDIA KUITANGAZA TANZANIA


Itatumia mapambano yake kutangaza vivutio vya kitalii vya Tanzania

■ Kila bondia atakayegombea taji lake atavaa nembo zenye vivutio vya kitalii vya Tanzania

Katika hali inayoashiria uzalendo wa hali ya juu, Shirikisho la Ngumi la Kimataifa bara la Afrika, Mashariki ya Kati na Ghuba ya Uajemi (IBF) litaanza kuvitangaza vivutio vya kitalii vya Tanzania katika mapambano yake yote ya ngumi ili viweze kujulikana zaidi ulimwengumi.


Katika program yake ya “Utalii wa Michezo” iliyowakilishwa na Rais wa shirikisho hilo katika bara la Afrika, Mashariki ya Kati na Ghuba ya Uajemi Mtanzania Onesmo Ngowi, na kukubaliwa na mkutano mkuu wa 29 wa Shirikisho la Ngumi la Kimataifa na Chama Cha Ngumi Cha Marekani (IBF/USBA) uliomalizika hivi punde jijini Honolulu, Hawaii programu ya "Utalii ya Michezo ya IBF" imegawanyika katika sehemu tatu:


1.    Utalii wa Mikutano ya IBF

2.   Utalii wa Kupanda Mlima Kilimanjaro kila mwaka (IBF Mount Kilimanjaro Climb Expedition)

3.    Utalii wa mapambano ya Ngumi


Ni katika “Utalii wa mapambano ya Ngumi” ambako shirikisho hili limeamua kuvitangaza vivutio vya kitalii vya Tanzania.


Hii ni mara ya kwanza kwa taasisi ya michezo hapa nchini na katika bara la Afrika kutumia mitandao yake kutangaza vivutio vya kitalii vya nchi ya Afrika.


Akitangaza nia ya IBF kuitangaza Tanzania duniani kote Rais wa shirikisho hilo katika bara la Afrika, Mashariki ya Kati na Ghuba ya Uajemi Onesmo Ngowi alisema kwamba ni muhimu sisi Watanzania tuliopewa nafasi katika taasisi za kimataifa tukatambua kuwa nchi yetu inatakiwa kutangazwa.


Kwa kuanzia kila bondia wa Kitanzania atakayewakilisha nchi hii na taarifa yake kuandikwa, taarifa hii itaanza na neo "MTANZANIA" halafu jina lake. Hii ni kuiweka nchi yetu mbele ya kila kitu na hii "BRANDING" kama inavyojulikana katika ulimwengu wa masoko na promosheni za biashara.


Katika mkakati huu MTANZANIA Ngowi alisema kuwa kwa sasa kuna mapambano kadhaa mbayo mabondia wa Kiafrika wanashiriki na watayatumia kutangaza vivutio cya kitanzania. Alisema kuwa bondia Helen Joseph wa Nigeria anayeishi Ghana atapambana na bondia Dahianna Santana wa nchi ya Dominican Repubic na Helen ataitangaza Tanzania.


Mpambano huo utafanyika nchini katika jiji la Santo Domingo nchini Dominican Republic, iliyoko katika eneo la Karibian karibu na Jamaica tarehe 12 August mwaka huu.


Aidha MTANZANIA Ramadhani Shauri atapambana na bondia Sande Kizito wa Uganda katika mpambano uliopewa jina la “The Rumble in the City” (Rurumai katika jiji) mpambano huo utafanyika siku ya Idd pili katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini dar-Es-Salaam.


Naye MTANZANIA Nasibu Ramadhani atapimana ubavu na bondia Twalib Mubiru wa Kenya kugombea mkanda wa IBF Afrika ya Mashariki na Kati katika uzito mwepesi (lightweight) siku hiyo hiyo ya Idd pili, jijini dar-Es-Salaam.


Aidha, MTANZANIA Rajabu Maoja anayeishi katika jiji la Tanga atapimana ubavu na bondia Gottlieb Ndokosho bingwa wa ngumi nchini Namibia kugombea mkanda wa IBF wa mabara katika uzito wa Unyoya. Mapambamo huo uliopewa jina la “The battle of the Kalahari Desert” (Vita vya Jangwa la Kalahari) utafanyika katika jiji la Windhoek nchini Namibia.

Naye MTANZANIA Allen Kamote atapimana ubavu na bondia Wilson Masamba wa Malawi katika mpambano wa kugombea mkanda wa IBF katika bara la Afrika uzito mwepesi "Lightweight" jijini Arusha tarehe 27 Octoba mwaka huu katika mpambano uliipewa jina la "TANZANITE Title" (Ubingwa wa Tanzanite). Mpambano huo utafanyika katika jiji la Arusha na utaandaliwa na bondia wa zamani wa taifa George Andrew chini ya kampuni yake ya


NIMEAMBATANISHA PICHA YA ONESMO NGOWI AKIWAKILISHA UTALII WA MICHEZO, HAWAII, MAREKANI

UCHAGUZI NETIBOLI


Uchaguzi netiboli Dar Agosti 11


Na Mwandishi Wetu
CHAMA cha Netiboli Mkoa wa Dar es Salaam (CHANEDA), kinatarajia kufanya uchaguzi wa viongozi wake Agosti 11, mwaka huu jijini.

Akizungumza na gazeti hili jijini jana, Ofisa Habari wa CHANEDA, Michael Maurus, alisema kuwa uchaguzi huo unafanyika, ikiwa ni baada ya viongozi waliopo madarakani kumaliza muda wao tangu mwaka jana.

Alisema kuwa kuchelewa kufanyika kwa uchaguzi huo kulitokana na vyama vya wilaya za Ilala, Kinondoni na Temeke kutofanya chaguzi zao ili kupata wapiga kura halali ambao ndio watakaochagua viongozi wa mkoa.

“Ili uchaguzi ufanyike, lazima kuwapo na wapiga kula halali ambao ni viongozi wa klabu na vyama vya netiboli vya wilaya, tuliagiza vyama vifanye chaguzi, lakini hadi sasa hakuna mwitikio wowote, hivyo tumeona tuwatumie viongozi wa klabu kufanya uchaguzi huo wa mkoa ili viongozi watakaopatikana wapange taratibu za kufuatilia kila chama cha wilaya kuona nini kinaendelea huko,” alisema Maurus.

Juu ya uchaguzi huo wa CHANEDA, Maurus alisema kuwa mchakato wa uchukuaji fomu na kurudisha, unaanza Jumatatu ya Julai 23 hadi Julai 30, mwaka huu wakati usaili itakuwa ni Agosti 4, mwaka huu.

Maurus alisema kuwa fomu za kuwania uongozi huo zinapatikana katika ofisi ya Ofisa Michezo Mkoa wa Dar es Salaam.

Kwa sasa viongozi waliobaki wanaokisimamia chama hicho ni Mwenyekiti Winfida Emmanuel, Katibu Mkuu Joseph Ng’anza na Maurus akiwa kama Ofisa Habari na Katibu Msaidizi.

Wengine waliokuwa na nafasi CHANEDA ambao hata hivyo hawakuwa karibu na chama hicho kutokana na sababu mbalimbali, ni Jackson Henzron (Mweka Hazina), Christina Kimamla, Mussa Sambala, Khadija Ally na Moshi Mganga (wote wajumbe), huku Makamu Mwenyekiti akiwa ni Pili Mogella ambaye hata hivyo alijiondoa kutokana na kutohudhuria vikao.

CELEBRITIES WITHOUT MAKEUP

 LADY GAGA
BEYONCE
 EVA

 PENELOPE CRUZ
 KATHERINE HEIGH
 KHLOE KARDASHIAN
 SNOOKI
 JLO
 HILAL DUFF

 PINK
 ANNE HATHWAY
 ANGELINA
 JLO
 KIM K
JESSICA BIEL

What do you think???

HAIR STYLES









PONGEZI KWA UONGOZI MPYA DOREFA

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linatoa pongezi kwa uongozi mpya wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dodoma (DOREFA) uliochaguliwa katika uchaguzi uliofanyika juzi (Julai 21 mwaka huu).
Ushindi waliopata viongozi waliochaguliwa kuongoza chama hicho unaonesha jinsi wajumbe wa Mkutano Mkuu wa DOREFA walivyo na imani kubwa kwao katika kusimamia mchezo huo mkoani Dodoma.
TFF inaahidi kuendeleza ushirikiano wake kwa Kamati ya Utendaji ya DOREFA chini ya uenyekiti wa Nasoro Kipenzi ambaye amechaguliwa kwa kipindi cha pili mfululizo.
 
Uongozi huo mpya una changamoto nyingi, kubwa ikiwa ni kuhakikisha unaendesha shughuli za mpira wa miguu mkoani Dodoma kwa kuzingatia katiba ya DOREFA pamoja na vyombo vya mpira wa miguu vilivyo juu yake.
Pia tunatoa pongezi kwa Kamati ya Uchaguzi ya DOREFA na Kamati ya Uchaguzi ya TFF kwa kuhakikisha uchaguzi huo unaendeshwa kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi za wanachama wa TFF.
Viongozi waliochaguliwa katika uchaguzi huo uliofanyika hoteli ya Dear Mama ni Nassoro Kipenzi (Mwenyekiti), Thadeo Kaliza (Makamu Mwenyekiti), Stewart Masima (Katibu Mkuu), Kepha Maswaga (Mhazini), Mulamu Ngh’ambi (Mjumbe wa Mkutano Mkuu TFF), Mohamed Aden (Mwakilishi wa Klabu TFF), Zawdi Kassim (Mjumbe Kamati ya Utendaji).

 
RAMBIRAMBI MSIBA WA MTANGAZAJI JOSEPH MAPUNDA
Shrikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko kifo cha mtangazaji wa michezo wa Radio Wapo, Joseph Mapunda kilichotokea juzi asubuhi (Julai 21 mwaka huu) jijini Dar es Salaam.
Msiba huo ni mkubwa katika sekta ya habari na mpira wa miguu kwani kwa nyakati tofauti Mapunda alifanya kazi na TFF kwa kuripoti shughuli zetu nyingi za mpira wa miguu, hivyo mchango wake tutaukumbuka daima.
TFF inatoa pole kwa familia ya marehemu Mapunda, Radio Wapo na Chama cha Waandishi wa Habari Tanzania (TASWA) na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito.
Mungu aiweke roho ya marehemu Mapunda mahali pema peponi. Amina