Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji mmoja wa walionusurika katika ajali ya meli jana huko Chumbwe wakati Rais na Mama Salma Kikwete walipowatembelea kuwafariji na kuwapa pole katika hospitali kuu ya Mnazi Mmoja Jana.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakitembelea Uwanja wa Maisara, Zanzibar, ambako ndiko miili ya marehemu
huletwa kwa utambuzi baada ya kuokolewa kwenye eneo la ajali jana
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakitembelea Uwanja wa Maisara, Zanzibar, ambako ndiko miili ya marehemu
huletwa kwa utambuzi baada ya kuokolewa kwenye eneo la ajali jana
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji mmoja wa walionusurika katika ajali ya meli jana huko Chumbwe wakati Rais na Mama Salma Kikwete walipowatembelea kuwafariji na kuwapa pole katika hospitali kuu ya Mnazi Mmoja jana.
Rais Jakaya Kikwete na Mama Salma Kikwete wakimsikiliza mmoja wa walionusurika katika ajali ya meli jana Bw Kitwana Makama Haji ambaye kalazwa katika hospitali kuu ya Mnazi Mmoja jana
Rais Jakaya Kikwete na Mama Salma Kikwete wakimpa pole Bi Salome Abeli, mmoja wa walionusurika katika ajali hiyo ya meli. Yeye ni mfanyakazi wa Tanzania Automic Energy Commission akitokea Arusha kwenda Pemba Kikazi jana.
Friday, July 20, 2012
Thursday, July 19, 2012
Kigoma all Stars Concert in Kigoma
wabunge on stage
makomando.
Umati.
Umati.
wabunge-halima na estherbulaya
zitto kabwe welcomes
zittojukwani
TAARIFA YA MHESHIMIWA DKT. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, KUFUATIA AJALI YA KUZAMA KWA MELI YA MV SKAGIT ILIYOTOKEA TAREHE 18 JULAI, 2012, CHUMBE, ZANZIBAR
THE
UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Jana tarehe 18 Julai,
2012, majira ya alasiri kumetokea ajali ya kuzama kwa meli ya MV SKAGIT katika
eneo la Chumbe, Zanzibar. Meli hiyo
iliyokuwa ikitokea Dar es Salaam kueleka Zanzibar ilikuwa imebeba watu 290. Kati yao watu wazima 250, watoto 31 na wafanyakazi wa meli 9.
Amiri
Jeshi Mkuu, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete aliagiza vyombo vya ulinzi na
usalama vya Serikali ya Muungano yaani JWTZ na
Polisi waanze kazi ya uokoaji mara moja.
Kazi hiyo imefanywa kwa kushirikiana
na vyombo vya usalama vya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na meli za makampuni
binafsi. Mpaka giza lilipokuwa limeingia
na hivyo kazi ya uokoaji kusitishwa mpaka kutakapokucha tarehe 19 Julai, 2012,
watu 136 walikuwa wameokolewa na
maiti 31 zilikuwa zimepatikana. Aidha, mali zilizokuwa kwenye meli hiyo
hazikuweza kuokolewa.
Kufuatia ajali hiyo, Rais wa Jamhuri
ya Muungano alizungumza na Dkt. Ali Mohamed Shein, Rais wa Serikali ya
Mapinduzi Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi. Alimpa pole kwa ajali iliyotokea hasa kwa
vifo na majeraha waliyopata Watanzania wenzetu na watu wasiokuwa raia wa
Tanzania. Alimuomba afikishe salamu za
rambirambi kwa ndugu zetu waliopotelewa na jamaa zao na kuwapa pole waliopata
majeraha na maumivu maungoni mwao. Rais wa Jamhuri ya Muungano alisema kuwa huu
ni msiba wetu sote na kwamba majonzi yao ni majonzi yake na ya Watanzania
wote. Kwa ndugu zetu waliojeruhiwa tunawaombea
kwa Mwenyezi Mungu awape ahueni na wapone haraka ili waweze kuendelea na
shughuli zao za kujiletea maendeleo na kulijenga taifa letu.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amempongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti
wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Ali Mohamed Shein na viongozi wote wa ngazi
mbalimbali kwa uongozi wao thabiti tangu taarifa ya kutokea kwa ajali mpaka
sasa. Aidha, amewapongeza maafisa na
askari wa vyombo vya ulinzi na usalama na wafanyakazi wa meli binafsi, kwa
juhudi kubwa walizozifanya za uokoaji wa ndugu zetu waliopatwa na maafa haya
makubwa na ya aina yake. Amewataka
waendeleze juhudi hizo leo na siku zijazo.
Rais amewataka wananchi wawe na moyo
wa subira na uvumilivu wakati kazi ya uokoaji inaendelea. Kama ilivyofanyika katika ajali ya MV Spice
Islander miezi 10 iliyopita, uchunguzi wa kina utafanyika kubaini chanzo cha
ajali.
Kutokana na ajali hiyo na msiba huu
mkubwa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho
Kikwete, ametangaza maombolezo ya taifa ya siku tatu ambapo bendera zitapepea
nusu mlingoti kuanzia leo, tarehe 19 Julai, 2012.
Asanteni
sana.
Imetolewa na:
Kurugenzi
ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar
es Salaam.
19 Julai, 2012
Wednesday, July 18, 2012
PICHA MBALI MBALI ZA MAAFA YA KUZAMA KWA MELI ZANZIBAR
Watalii na raia wa kigeni pia walikuwemo katika meli iliyozama hawa ni baadhi ya
waliosalimika
Mtoto aliyeokoka kutoka katika meli iliyozama
Abiria aliyeokoka kutoka katika meli iliyozama
Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Hamad Masoud Hamad akiwa katika hali ya
huzuni Baada ya kushiriki katika uokoaji na kuwaona Majeruhiwaliookolewa katika
Meli iliozama ya Star Gate wakiteremka hapo Bandarini Zanzibar
BREAKING NEWS: MELI YA MV KARAMA INASEMEKANA KUZAMA ENEO LA CHUMBE VISIWANI ZANZIBAR
Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana
kupitia kwa mashuhuda Meli hiyo MV Karama ya Kampuni ya Seagal imezama baada ya
kupinduka kichwa chini miguu juu katika eneo la Chumbe karibia na Visiwa vya
Zanzibar.
Mashuhuda hao wanakisia kuwa takribani watu
200 walikuwa ndani ya meli hiyo hata hivyo watu kadhaa wameonekana wakiwa
wanelea huku wakiwa wamevaa (Life Jackets) na kuwa boti zisizopungua 4
zimeshafika eneo la tukio kwa ajili ya kuwaokoa na Wahanga wa ajali hiyo
wamepelekwa katika Hospitali ya Mnazi Mmoja
MASANJA MKANDAMIZAJI AWASHA MOTO IRINGA MJINI KATIKA UZINDUZI WA ALBAM YAKE YA HAKUNA JIPYA
Mungu alimtumia Emmanuel Mgaya (Masanja Mkandamizaji au Mchungaji Mtarajiwa) kuwakusanya watu katika Uwanja wa Samora mjini Iringa kushuhudia matendo makuu ya Mungu, ambapo msanii huyu alikuwa akizindua albamu yake ya "Hakuna Jipya" Masanja Mkandamizaji ni mkazi wa jijini Dar es Salaam ni mzawaliwa wa mkoa wa Iringa. Aliamua kufanya tamasha lake katika mkoa aliozaliwa.
Msanja Mkandamizaji aliwakusanya watu kutoka mikoa mbalimbali waliofika kushuhudia uzinduzi huo. Wasanii wa filamu za kibongo kutoka Dar es Salaam walifika mahali pale kama. Odama, Ray, steve Nyerere, Davina, Chopa Mchopanga, Jacquline Wolper na wengine wengi walifika mahali pale.
Mbali na uimbaji masanja Mkandamizaji ni mchekeshaji katika kituo cha televisheni cha TBC1 "Orijino ze Commedy", kutokana na karama hiyo ya uchekeshaji amepata kibali cha kukubalika katika jamii.
Masanja kwa sasa anajiita "Mchungaji Mtarajiwa" anategemea kuwa mchungaji lakini anasema hajui itakuwa saa ngapi, siku gani na wapi ataanza huduma hiyo, ila anakuomba uzidi kumuombea.
Msanja Mkandamizaji aliwakusanya watu kutoka mikoa mbalimbali waliofika kushuhudia uzinduzi huo. Wasanii wa filamu za kibongo kutoka Dar es Salaam walifika mahali pale kama. Odama, Ray, steve Nyerere, Davina, Chopa Mchopanga, Jacquline Wolper na wengine wengi walifika mahali pale.
Mbali na uimbaji masanja Mkandamizaji ni mchekeshaji katika kituo cha televisheni cha TBC1 "Orijino ze Commedy", kutokana na karama hiyo ya uchekeshaji amepata kibali cha kukubalika katika jamii.
Masanja kwa sasa anajiita "Mchungaji Mtarajiwa" anategemea kuwa mchungaji lakini anasema hajui itakuwa saa ngapi, siku gani na wapi ataanza huduma hiyo, ila anakuomba uzidi kumuombea.
Masanja akisindikizwa na waimbaji mbalimbali kutoka Iringa na mikoa mingine katika uwanja wa samora mjini Iringa
Masanja Makadamizaji akikagua gwaride lake
Waimbaji wakiwa pamoja na Masanja Mkandamizaji aliyeshika ubao kama alama ya bunduki
Hapa Mgeni Rasmi akiongea baada ya kuzindua waliokaa ni baadhi ya wabunge wa viti maalum na mkuu wa mkoa wa Iringa.
JB wa Bongo Movie akiwa ameshika kibaza sauti pamoja na waigizaji wenzake
JB toka bongo movie akitoa support kwa kununua DVD na Audio Cd
Diwani wa kata ya kitanzini Manispaa ya Iringa Jesca hakuwa nyuma kutoa support kwa kununua DVD ya album ya HAKUNA JIPYA
Masanja Mkandamizaji na gwaride lake wakiingia jukwaani
Naibu Waziri wa Elimu Milubo akizindua DVD na VCD
Vicent Kigosi (Ray) akisalimia wakazi wa Iringa
Jacquline Waolper akiwa na furaha kuona tamasha linaenda vizuri
Subscribe to:
Posts (Atom)