Saturday, August 11, 2012

REHMTULLAH KUZINDUA MITINDO MIPYA

Mwanamitindo maarufu hapa nchini Ally Rehmtullah ameandaa onyesho kubwa na la kipekee la mitindo hapa nchini litakalofanyika tarehe 8 Mwezi ujao katika jiji la Dar es Salaam na litarushwa moja kwa moja katika mtandao wa www.ar.co.tz bure kabisa ambapo atazindua rasmi kazi zake mpya za mitindo ya mavazi mbalimbali kwa wanaume na wanawake.
Akizungumza na vyombo mbalimbali vya habari hivi karibuni, Rehmtullah alisema dhumuni la kuandaa onyesho hilo la kipekee ni kuweza kuonyesha aina mpya ya mitindo ya mavazi aliyobuni hivi karibuni na harakati zake za kuinua kiwango cha kazi za mitindo ndani ya nchi.“Nimepania kupanua wigo wa taaluma ya mitindo na mavazi hapa nchini ili kazi za wanamtindo na wabunifu wa mavazi hapa nchini ziweze kupenya kwenye soko la ndani na la Afrika mashariki na ya kati wakati tayari kuna soko la pamoja katika jumuiya ya Afrika mashariki,’ alisema.                                                                            Rehmtullah alisema kwamba onyesho hilo litakuwa la kipekee kwa sababu mavazi na onyesho litapambwa na rangi nyeupe,ubunifu wa hali ya juu pamoja na muonekano mpya wa mavazi yaliyofanyiwa utafiti mkubwa ili kuweza kuendana na utamaduni wa mwafrika.
Alisema onyesho hilo ambalo litafanyika katika hoteli ya Serena litapambwa na wasanii mbalimbali wa muziki na wacheza shoo toka sehemu mbalimbali hapa nchini.                                          Rehmtullah alisema onyesho hilo itakuwa ni nafasi ya kipekee kwa yeye binafsi kuonyesha muonekano mpya wa tasnia ya mitindo hapa nchini na nje ya nchini ili kuonyesha ni kwa jinsi ngani wanamitindo wa kitanzania wanavyoweza kuonyesha kazi zao. Alisema kuwa tasnia ya mitindo kwa ujumla ina nafasi ya kipekee kwa wanamtindo chipukizi hapa nchini kujitokeza na kuonyesha kazi zao kwa watu mbalimbali hasa washika dau katika sekta hiyo.
‘kazi za mitindo na mavazi ndio mkombozi wa kweli katika kupunguza tatizo la ajira nchini Tanzania kwa sababu ni sekta inayokua kwa kasi kubwa na inatoa ajira kwa vijana wengi wa kike na kiume,’aliongeza Onyesho hilo linategemewa kuhudhuriwa na watu zaidi ya 400 wakiwemo viongozi mbalimbali kama mawaziri, wabunge, wakuu wa wilaya, wakurugenzi wa mashirika mbalimbali. Onyesho hilo litakuwa ni la mialiko maalum na limepewa jina la Ally Rehmtullah 2013 collection.               Wadhamini wa onyesho hilo ni Mercedez Benz, Belvedere Vodka, DULUX, RAHA, HUGO DOMINGO,THE Tanzanite Experience, Shiva Images, Farm Plant, Creative Infinities, Out Door, Stanbic Bank, Phoenicia Properties, Dar es Salaam Serena Hotel, Missie Popular Blog, Mo Blog, Quality Furniture na Mx Carter




RAIS KIKWETE KATIKA MAZISHI YA RAIS JOHN ATTA MILLS WA GHANA

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisaini kitabu cha maombolezo wakati shughuli ya mazishi ya Rais John Evans Atta Mills wa Ghana katika ukumbi wa Mikutano wa Ghana jijini Accra leo Agosti 10, 2012.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisaini kitabu cha maombolezo wakati shughuli ya mazishi ya Rais John Evans Atta Mills wa Ghana katika ukumbi wa Mikutano wa Ghana jijini Accra leo Agosti 10, 2012.
 Shughuli mbalimbali za  mazishi za aliyekuwa Rais wa Ghana Profesa John Evans Atta Mills katika uwanja wa Independence Square jijini Accra leo Agosti 10, 2o12
 Shughuli mbalimbali za  mazishi za aliyekuwa Rais wa Ghana Profesa John Evans Atta Mills katika uwanja wa Independence Square jijini Accra leo Agosti 10, 2o12
 Shughuli mbalimbali za  mazishi za aliyekuwa Rais wa Ghana Profesa John Evans Atta Mills katika uwanja wa Independence Square jijini Accra leo Agosti 10, 2o12
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na viongozi wenzie  baada ya shughuli ya mazishi ya Rais John Evans Atta Mills wa Ghana jijini Accra leo Agosti 10, 2012

Lisa Jensen Miss World



Mwakilishi wa Tanzania katika mashindano ya urembo ya Dunia ya Miss World, Lisa Jensen akiwa katika matukio mbalimbali mjini Ordos, China kunakofanyika maandalizi wa mashindano hayo

Victoria & David Beckham with baby Harper...fashionable family

Thursday, August 9, 2012

Miss Tanzania akiwa Miss world

Mrembo Lisa Jensen anayeiwakilisha Tanzania katika mashindano ya urembo ya Dunia Miss World 2012, akiwa na baadhi ya washiriki wa Mashindano hayo, mjini Ordos China, jana

Wednesday, August 8, 2012

IBF/USBA YAONGEZA TAJI JIPYA KWA MABONDIA WA AFRICA, MASHARIKI YA KATI

Katika mpango wake kabambe wa kupanua wigo wa mabondia wa “Kiafrika, Mashariki ya Kati na Ghuba ya Uajemi” kujitangaza katika tasnia ya ngumi za kulipwa, Shirikisho la Ngumi la Kimataifa na Chama Cha Ngumi Cha Marekani (IBF/USBA) limezindua taji jipya.

 Taji hilo linajulikana kama “Ubingwa wa IBF Afrika, Mashariki ya Kati na Ghuba ya Uajemi” kwa kizungu ni “IBF Africa, Middle East and Persian Gulf Title” au (IBF/AMEPG).

 Mpamnano wa kwanza wa ubingwa huo utafanyika katika jiji la Windhoek nchini Namibia Septemba 1, 2012 kati ya “Mtanzania Rajabu Maoja” na bingwa wa Namibia Gottlieb Ndokosho!

Mpambano mwingine unategemewa kufanyika katika jiji la Accra nchini Ghana kati ya bondia Richard Commey wa Ghana ambaye kwa sas aanajifua nchini Uingereza na bondia kutoka nchi ya Qatar ambayo iko katika Ghuba ya Uajemi.

 Juhudi hizi za IBF/USBA zinakuja wakati ambapo shirikisho hili limeanzisha programu ya “Utalii wa Michezo” na kuziteua Tanzania na Ghana kama nchi za mfano kwa kipindi cha miaka mitatu (3).

 Akizungumzia kuhusu taji hilo jipya Rais wa “IBF/USBA katika bara la Afrika, mashariki ya Kati na Ghuba ya Uajemi” Mtanzania Onesmo Ngowi alisema kuwa mabondia wa Kitanzania wanatakiwa kuzichangamkia fursa hizi ili kuweza kujiweka katika nafasi nzuri ya kuweza kugombea mataji ya juu zaidi.

Ngowi alibainisha kuwa kwa sasa ni mabondia wachache sana wa Tanzania ambao wana viwango vya juu ukilingamisha na mabondai wan chi za Ghana, Namibia, Afrika ya Kusini, Uganda, Nigeria na Misri.

Aliahidi kuwapatia mabondia wa kiatnzania nafasi za kugombea mataji haya kila panapotokea nafasi hizi.

Utawala

IBF/USBA Afrika, Mashariki ya Kati na Ghuba ya Uajemi

Tuesday, August 7, 2012

Big Brother StarGame Finale: Day 91 pictures

 BBA winner Keagan
 Talia and IK
 Lady Mary and IK
 Chris and Julio
 South Africa’s Kuli Chana
 BBA winner Keagan
 Lady Mary and IK
Prezzo and IK


Monday, August 6, 2012

WHO IS THE SEXIER LADY IN RED

Two different red hot looks, two different Hollywood ladies.
Reality TV star Kate Gosselin was spotted strolling around New York on August 4, donning a sleeveless, fitted red dress.
Carrying a feminine nude shoulder bag, the blonde mother-of-eight, 37, showed off her sunkissed glow while still staying conservative.
She looked great — and apparently felt great too — flashing a big smile for the camera.
But how does Gosselin compare to another lady in red?

Britney Spears n Kim kardashian

HAPPY 2ND ANNIVERSARY TO MY GIRL NARGIS N THE HUSBY

May god bless you guys with hundred years together

TENGA KUFUNGUA KOZI YA UONGOZI YA FIFA

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) anatarajia kufungua Kozi ya Uongozi na Utawala ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) inayoanza leo (Agosti 6 mwaka huu) Msimbazi Center jijini Dar es Salaam.

Kozi hiyo itakayokuwa na washiriki zaidi ya 30 itamalizika Agosti 11 mwaka huu na itaendeshwa na Wakufunzi kutoka FIFA na itafunguliwa saa 3 asubuhi. Wakufunzi hao ni Barry Rukoro anayetoka Namibia, Henry Tandau (Tanzania) na Senka Kanyenvu (Botswana).

Baadhi ya washiriki wa kozi hiyo ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa TFF, Athuman Nyamlani, Rais wa ZFA Amani Makungu, wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF; Ahmed Mgoyi, Blassy Kiondo, Stanley Lugenge, Khalid Abdallah, Hussein Mwamba na Eliud Mvella.

Wengine ni Katibu Mkuu wa ZFA, Kassim Salum, Katibu Msaidizi wa ZFA, Masoud Attai, wenyeviti wa vyama vya mpira wa miguu vya mikoa ya Kagera (Jamal Malinzi), Dodoma (Nassoro Kipenzi) na Pascal Kihanga (Morogoro).

Makatibu wa vyama vya mpira wa miguu vya mikoa ya Mara (Mugisha Galibona), Mtwara (Vincent Majiri), Morogoro (Hamisi Semka), Kagera (Salum Chama), Tanga (Beatrice Mgaya) na Dodoma (Stuart Masima). Pia yumo Mwenyekiti wa Coastal Union, Ahmed Hilal na Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga.

Washiriki wengine ni Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah, Mkurugenzi wa Ufundi, Sunday Kayuni, Ofisa Habari, Boniface Wambura, Mkurugenzi wa Masoko na Matukio, Jimmy Kabwe na Mkurugenzi wa Mashindano, Saad Kawemba.

Wengine ni Ofisa Sheria wa TFF, Neema Lucumay, Ofisa wa Mpira wa Miguu wa Wanawake, Grace Buretha, Amina Karuma (Mpira wa miguu wa wanawake) na nahodha wa zamani wa Taifa Stars, Shadrack Nsajigwa.

Sunday, August 5, 2012

KEAGAN FROM SOUTH AFRICA IS THE WINNER OF BIG BROTHER STAR GAME 2012, WALK AWAY WITH US$300, 000.

 South African Housemate Keagan has won the Big Brother StarGme!
After 91 long days in the house, the young lad has finally hit the jack pot. His journey started in Doenville with partner Lee who was evicted on the same night he was Upgraded to Upville.
This means that South Africa has won Big Brother for the first time after a long wait.
The South African housemate managed to beat off stiff competition from 34 other housemates including strong contenders from Upville.
Prezzo was the runner up and was rewarded with a ONE Campaign ambassador slot. He was also told that he would be attending Jay Z’s concert in the United States soon.


How Africa Voted!

South Africa’s Keagan wins StarGame! (5th August 2012, week 12)
Here’s who which country voted for:
Angola: Keagan
Botswana: Keagan
Ghana: Keagan
Kenya: Prezzo
Liberia: Keagan
Malawi: Wati
Namibia: Lady May
Nigeria: Keagan
South Africa: Keagan
Sierra Leone: Talia
Tanzania: Prezzo
Uganda: Kyle
Zambia: Talia
Zimbabwe: Lady May
Rest of Africa: Keagan
Total: Keagan = 7; Lady May = 2; Prezzo =2, Talia = 2, Kyle = 1, Wati = 1. (Total: 15 Votes)