Wednesday, September 5, 2012

REDD'S MISS TEMEKE 2012 WAANZA KUJINOA

VIMWANA 15 wa Redd's Miss Temeke, juzi wameanza rasmi kambi yao katika Club ya TCC Chang'ombe tayari wa kinyang'anyiro cha kanda hiyo, kumrithi mrembo Husna Twalib anayeshikilia taji hilo.
Warembo hao ambao wameanza programu ya shoo kwa wiki hii, chini ya ukufunzi wa Dickson Daud kutoka kikundi cha THT, wanatoka katika vitongoji vya Kigamboni, Kurasini na Chang'ombe ambapo kila sehemu wametoka warembo watano ambapo washindi watatu wa kwanza watapata fursa ya moja kwa moja kushiriki Redds Miss Tanzania 2012.
Warembo hao ni Agness Goodluck, Angela Gasper, Flaviana Maeda,Edna Sylvester, Catherine Masumbigana, Khadija Kombo, Neema Doreen, Flora Kazungu, Lilian Joseph, Elizabeth Peter, Elizabeth Boniphace, Jesca Haule, Zulfa Bundala, Mariam Ntakisivya na Esther Albert.
Temeke imewahi kutwaa taji la Miss Tanzania mara tatu, kupitia warembo Happiness Sosthenes Magesse aka Millen mwaka 2001, Sylvia Remmy Baham mwaka 2003 na Genevieve Mpangala. Lakini pia imetoa warembo waliowahi kushika nafasi ya pili na tano bora katika Miss Tanzania kama Jokate Mwegelo, Irene Uwoya, Irene Kiwia, Queen David, Cecylia Assey, Sabrina Slim, Miriam Odemba, Ediltruda Kalikawe na Asela Magaka.
Mbali ya Redd's, Miss Temeke 2012 pia imedhaminiwa na Dodoma Wine, gazeti la Jambo Leo, Push Mobile, City Sports Lounge, 100.5 Times FM, Kitwe General Traders na 88.4 Times FM. Warembo wanaendelea na mazoezi na leo, Agosti 5 wanatarajia kutembelewa na Miss Tanzania 2010, Genevieve Mpangala ambaye pia ni Miss Temeke wa mwaka huo.
 Mkufunzi wa warembo katika shoo ya Redd's Miss Temeke, Dickson Daud akiwanoa warembo hao katika Club ya TCC Chang'ombe jana, tayari kwa shindano lao litakalofanyika Septemba 21 mwaka huu.

Warembo wa Redd's Miss Temeke, wakiwa mazoezini jana katika Club ya TCC Chang'ombe , tayari kwa shindano lao litakalofanyika Septemba 21 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment