Monday, September 3, 2012

MADIWANI KG'MBONI WAWAPA TAFU WAREMBO WAO MISS TEMEKE

 Diwani wa Kata ya Kibada, Juma Nkumbi (wa tatu kulia), akimkabidhi Sh.milioni 1 Mratibu wa Reds Miss Kigamboni 2012, Somoe Ng'itu ikiwa mchango wa madiwani wa Kigamboni kwa warembo wa kata hizo kwa ajili ya maandalizi ya ushiriki wao kwenye mashindano ya Redd's Miss Temeke 2012 ambao jana walianza mazoezi kwenye club ya TCC Chang'ombe. Wa tatu kushoto ni Diwani wa Kata ya Vijibweni Suleiman Mathew, mwingine aliyechangia warembo hao ni diwani wa Kigamboni Dotto Msawe.
Warembo wa Reds Miss Kigamboni wanaoiwakilisha kitongoji hicho kwenye Miss Temeke kutoka kushoto ni Khadija Kombo, Elizabeth Biniface, Agnes Goodluck, Esther Albert na Eda Sylvester.

No comments:

Post a Comment