Friday, June 29, 2012

RAY AZINDUA FILAMU YA SOBING SOUND KWA KUTOA MSAADA AKISHIRIKIANA NA STEPS

MSANII wa filamu nchini Vicent Kigos 'Ray' amezindua filam yake mpya inayojulikana kama 'SOBING SOUND'.

Filam hiyo ameizindua kwa staili tofauti ambapo badala ya kuzindua Ukumbini kama ilivyozoeleka na wengi, msanii huyo amezindua filam hiyo katika kituo cha watoto yatima cha Maunga Centre kwa kutoa msaada wa vitu mbalimbali vyenye thamani ya sh. milioni 1.5 kwa niaba ya Kampuni ya Steps Entertainment ya jijini Dar es salaam

Akizungumza mara baada ya kuzindua filamu hiyo akiwa pamoja na watoto yatima wa kituo hicho, Ray alisema ameamua kufanya hivyo kutokana na ukweli kwamba watu wengi wamekuwa wakifurahia maisha huku wengine wakiendelea kutaabika kitendo ambacho si kizuri.

Alisema ujio wa filamu hiyo ni kama azma yake aliyoipanga tangu awali kuhakikisha filamu zake zote zinafanya vizuri na atakuwa kila filamu anayotoa atahakikisha japo kidogo kwa namna yoyote anawakumbuka watoto yatima.

Alisema msaada uliotolewa kwa watoto yatima hautaishia kwao bali ataendelea kutoa kile atakachokipata kupitia filamu hiyo kuwasaidia na wale wasiojiweza amesema kampuni ya Steps Entertaiment imekuwa msaada mkubwa kwa wasanii kutambulika na kushawishi wawe wanawakumbuka watoto wanaoishi katika mazingira magumu.

Msanii wa filamu nchini Vicent Kigosi 'Ray' akikadhi sehemu ya msaada uliotolewa na Kampuni ya Steps Entertainment ya jijini Dar es salaam leo kwa Mlezi wa kituo cha Maunga Centre Zainabu Bakari vyakula mbalimbali kushoto ni Meneja Masoko wa Kampuni ya Steps, Ignatus Kambarage

 Msanii wa filamu nchini Vicent Kigosi 'Ray' akikadhi sehemu ya msaada uliotolewa na Kampuni ya Steps Entertainment ya jijini Dar es salaam leo kwa Mlezi wa kituo cha Maunga Centre, Kinondoni, Dar es Salaam, Zainabu Bakari vyakula mbalimbali vya Tsh milioni 1.5 katika kituo hicho. kushoto ni Meneja Masoko wa Kampuni ya Steps, Ignatus Kambarage


Msanii wa Filamu Nchini Visent Kigosi 'Ray' katikati na Meneja Masoko wa Kampuni ya Steps.Ignatus Kambarage wakiwa katika picha ya pamoja baada ya lei kugawa vyakula mbalimbali katika kituo cha kulelea watoto yatima cha Maunga Centre .

No comments:

Post a Comment