Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Kimarekani na
waalimu wao pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa Mhe John Haule, Balozi wa Marekani nchini, Mhe na Balozi wa Tanzania
nchini Marekani Mhe Mwanaidi Sinare Maajar. Wanafunzi hao wanachukua masomo ya
lugha ya Kiswahili katika Chuo Kikuu cha Zanzibar ( SUZA). Walikuwa
wameongozana na Watendaji Wakuu wa Makampuni mbalimbali kutoka Marekani
walipomtembelea Rais Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam Juni 30, 2012
katika ziara yao ya siku kadhaa ya kuvumbua tanzania (Discover Tanzania VIP CEOs
tour iliyoandaliwa na ubalozi wa Tanzania Marekani
Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja na Watendaji Wakuu wa
Makampuni mbalimbali kutoka Marekani walipomtembelea Ikulu jijini Dar es salaam
leo Juni 30, 2012 katika ziara yao ya siku kadhaa ya kuvumbua tanzania (Discover
Tanzania VIP CEOs tour) iliyoandaliwa na ubalozi wa Tanzania Marekani. Hii ni
mara ya pili kufanyika ziara kama hii, ambapo pamoja na kuwakaribisha tena Rais
Kikwete alisema amefurahishwa sana kwa wageni hao kuchagua kutembelea hifadhi za
wanyama za kusini mwa nchi (Selous na Ruaha) vyenye wanyama wengi na vivutio
ambavyo havipatikani kwingine kokote kama vile makundi ya mbwa mwitu ambayo kwa
muda mrefu sasa yametoweka mbuga za Kaskazini.
No comments:
Post a Comment