Wednesday, July 18, 2012

BREAKING NEWS: MELI YA MV KARAMA INASEMEKANA KUZAMA ENEO LA CHUMBE VISIWANI ZANZIBAR


Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana kupitia kwa mashuhuda Meli hiyo MV Karama ya Kampuni ya Seagal imezama baada ya kupinduka kichwa chini miguu juu katika eneo la Chumbe karibia na Visiwa vya Zanzibar.

Mashuhuda hao wanakisia kuwa takribani watu 200 walikuwa ndani ya meli hiyo hata hivyo watu kadhaa wameonekana wakiwa wanelea huku wakiwa wamevaa (Life Jackets) na kuwa boti zisizopungua 4 zimeshafika eneo la tukio kwa ajili ya kuwaokoa na Wahanga wa ajali hiyo wamepelekwa katika Hospitali ya Mnazi Mmoja

1 comment: