Monday, July 16, 2012

MANJI, SANGA MABOSI WAPYA YANGA

Akitangaza matokeo, majira ya saa 10:30 alfajiri yab leo Julai 16,katika ukumbi wa Diamond Jubilee, Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi wa klabu ya Yanga Jaji John Mkwawa amemtangza Manji kama mshindi wa nafasi ya uenyekiti kwa kupata asilimia 97% ya kura zote zilizopigwa katika nafasi hiyo.
Nafasi ya Makamu mwenyekiti imekwenda kwa nahodha wa timu ya Yanga ya Gymkhana, Clement

Sanga aliyejipatia asilimia 62% ya kura zote zilizopigwa katika nafasi hiyo.
Katika nafasi ya Ujumbe wa kamati ya utendaji, wanachama Abdallah Bin Kleb, Moses Katabaro, Aaron Nyanda na George Manyama wamechaguliwa kushika nafasi hizo, baada ya kuwazidi wapinzani wao.

Jaji John Mkwawa amewashukuru wana Yanga kwa kuwa wastaarabu na watulivu, kitu kilicholekea kufanyika uchaguzi huo kwa amani na kumalizika salama pasipo kuwa na vurugu zozote.
Matokeo kamili ya wagombea ni: 

Nafasi ya Mwenyekiti:
Yusuf Manji  (kura 1876)  97.0%,  John Jembele (kura 40) 2.6%,  Edgar Chibura (kura 4) 0.24%

Nafasi ya Makamu Mwenyekiti:
Clement Sanga (kura 1948) 62.6%, Yono S Kevela (kura 475) 23%,  Ayoub Nyenzi (kura 288) 14%

Nafasi ya Ujumbe:
Abdallah Bin Kleb (kura 1942), Moses Katabaro (kura 1068),  Aaron Nyanda (kura 922), Geroge Manyama (kura 682), Beda Tindwa (kura 391), Edgar Fongo (kura 295),  Graticius Ishengoma (kura 247),  Jumanne Mwamenywa (kura 251),  Justine Baruti (610),  Lameck Nyambaya (kura 425),  Omary Ndula (kura 170),  Peter Haule (441),  Ramadhan Said (249),  Yono Kivela (123)
kutokana na matokeo yalivyo hapo juu safu ya viongozi waliochaguliwa ni
Mwenyekiti: Yusuf Manji,
Makamu Mwenyekiti: Clement Sanga
Wajumbe: Abdallah Bin Kleb, Moses Katabaro, Aaaron Nyanda, Geroge Manyama

 Clement Sanga(kushoto) na Yusuph Mehboob Manji



 Wanachama wa Yanga, Mzee Yusuph na mmiliki wa Global Publishers, Eric Shigongo
Mchezaji wa zamani Yanga, Aooron Nyanda ameshinda ujumbe

No comments:

Post a Comment