Tuesday, October 9, 2012

MISS MANYARA ATINGA 16 BORA MISS TZ

MREMBO,  Lucy Stephano juzi usiku alifanikiwa kukata tiketi ya kuingia 16 bora ya Redd’s Miss Tanzania, baada ya kufanikiwa kutwaa taji la mrembo mwenye mvuto na muonekana mzuri zaidi katika picha (Miss Photogenic).

 
Katika shindano  hilo lililofanyika katika ukumbi wa E’Manyata Lodge mjini Monduli, ushindani mkubwa ulikuwa kati yake na Miss us Miss Dar Indian Ocean, Diana Hussein na mshindi wa pili wa Miss Ilala , Magdalena Roy.

 
Kwa kufanikiwa kwake kutwaa taji hilo, Lucy ambaye ni mrembo wa mkoa Manyara na mwakilishi wa kanda ya Kaskazini amejipatia tiketi ya moja kwa moja ya kuingia 16 bora ya Miss Tanzania, akiwa mrembo wa kwanza kujihakikishia nafasi ya juu ya fainali ya Miss Tanzania  Novemba 3 mwaka huu, yatakayofanyika Ubungo Plaza.

 Shindano jingine dogo la kupata mrembo atakayefuatia kuingia 16 bora, linatarajiwa kufanyika Jumamosi  ili kumpata mwanamitindo bora ‘Top model’ wa Tanzania 2012, shindano litakaloitwa usiku wa Redd’s Miss Tanzania likifanyika Naura Spring mjini, Arusha.

 Warembo walioingia tano bora kutoka kulia Madgalena Roy(City Center-Ilala), Babylove Kalala(Kagera-Kanda Ziwa), Lightness Michael(Dodoma-Kati Kanda), Lucy Stephano(Manyara-Kanda Kaskazini) na Diana Hussein( Indian Ocean-Kinondoni)
Mkurugenzi wa Miss Tanzania, Hashim Lundenga akitangaza mshindi wa Miss Photogenic mbele ya warembo walioingia tano bora.

 

No comments:

Post a Comment