Thursday, July 12, 2012

MATUKIO MBALIMBALI YA ZIARA YA RAIS KIKWETE NCHINI UINGEREZA

 Rais Jakaya Mrisho kikwete, Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda na mkewe Mama Janet Museveni, Waziri Mdogo wa Uingereza wa Maendeleo ya Kimataifa Bw. Stephen O'Brien (kulia) na Mama Melinda Gates wakibadilishana mawazo kabla ya kuhutubia katika mkutano wa kimataifa wa viongozi kujadili Uzazi wa Mpango kwa nchi masikini zaidi duniani katika ukumbi wa Queen Elizabeth II jijini London July 11, 2012. Mkutano huo ni wa kwanza wa aina yake duniani na umeanzisha Mchakato wa Dunia ambao utalenga kuwawezesha wanawake wapatao milioni 120 katika nchi masikini zaidi duniani kupata habari, huduma na mahitaji ya kupanga uzazi bora zaidi na kuokoa maisha yao ifikapo mwaka 2020.

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akuhutubia katika mkutano wa kimataifa wa viongozi kujadili Uzazi wa Mpango kwa nchi masikini zaidi duniani, katika ukumbi wa Queen Elizabeth II jijini London July 11, 2012. Mkutano huo ni wa kwanza wa aina yake duniani na umeanzisha Mchakato wa Dunia ambao utalenga kuwawezesha wanawake wapatao milioni 120 katika nchi masikini zaidi duniani kupata habari, huduma na mahitaji ya kupanga uzazi bora zaidi na kuokoa maisha yao ifikapo mwaka 2020.

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Waziri Mkuu wa Uingereza Bw. Donald Cameron, Rais Paul Kagame wa Rwanda na Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda wakijiandaa kupanda jukwaani kuhutubia katika mkutano wa kimataifa wa viongozi kujadili Uzazi wa Mpango kwa nchi masikini zaidi duniani. katika ukumbi wa Queen Elizabeth II jijini London July 11, 2012. Mkutano huo ni wa kwanza wa aina yake duniani na umeanzisha Mchakato wa Dunia ambao utalenga kuwawezesha wanawake wapatao milioni 120 katika nchi masikini zaidi duniani kupata habari, huduma na mahitaji ya kupanga uzazi bora zaidi na kuokoa maisha yao ifikapo mwaka 2020.

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wake katika mazungumzo na Afisa Mtendaji Mkuu wa British Gas (BG Group), Sir Frank Chapman (wa pili kulia) na maafisa waandamizi wa kampuni hiyo. BG Group imewekeza kiasi cha Pauni 80 za Uingereza (Shilingi Trilioni 125) katika mradi wa kuchimba gesi asilia nchini Tanzania, na tayari visima vitano vya nishati hiyo vimeshatema gesi nyingi katika bahari kuu kusini mwa Tanzania maeneo ya Mtwara. Hii ilikuwa ni ziara fupi katika makao makuu ya BG Group mjini Reading, Uingereza ambako Rais Kikwete na ujumbe wake walitembelea Julai 11 kujionea namna kazi za uvumbuzi wa gesi asilia unavyofanywa na kampuni hiyo yenye kufanya shughuli zake katika nchi 21 katika mabara matano, ikiwa na jumla ya wafanyakazi 6,000.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na  Afisa Mtendaji Mkuu wa British Gas (BG Group), Sir Frank Chapman alipotembelea makao makuu ya kampuni hiyo mjini Reading Uingereza Julai 11, 2012. BG Group imewekeza kiasi cha Pauni 80 za Uingereza (Shilingi Trilioni 125) katika mradi wa kuchimba gesi asilia nchini Tanzania, na tayari visima vitano vya nishati hiyo vimeshatema gesi nyingi katika bahari kuu kusini mwa Tanzania maeneo ya Mtwara. Hii ilikuwa ni ziara fupi katika makao makuu ya BG Group mjini Reading, Uingereza ambako Rais Kikwete na ujumbe wake walitembelea Julai 11 kujionea namna kazi za uvumbuzi wa gesi asilia unavyofanywa na kampuni hiyo yenye kufanya shughuli zake katika nchi 21 katika mabara matano, ikiwa na jumla ya wafanyakazi 6,000.

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wakipata maelezo ya maendeleo ya uchimbaji wa gesi asilia nchini Tanzania walipotembelea makao makuu ya British Gas (BG Group), ambayo  imewekeza kiasi cha Pauni 80 za Uingereza (Shilingi Trilioni 125) katika mradi wa kuchimba gesi asilia nchini Tanzania, na tayari visima vitano vya nishati hiyo vimeshatema gesi nyingi katika bahari kuu kusini mwa Tanzania maeneo ya Mkoa wa Pwani na Mtwara. Hii ilikuwa ni ziara fupi katika makao makuu ya BG Group mjini Reading, Uingereza, ambako Rais Kikwete na ujumbe wake walitembelea Julai 11 kujionea namna kazi za uvumbuzi wa gesi asilia unavyofanywa na kampuni hiyo yenye kufanya shughuli zake katika nchi 21 katika mabara matano, ikiwa na jumla ya wafanyakazi 6,000.

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri Mdogo wa Maendeleo ya Kimataifa wa Uingereza Bw. Stephen O'Brien jijini London, ambapo Uingereza iliahidi kuendelea kuisaidia Tanzania katika mambo mbalimbali ya maendeleo ikiwa ni pamoja na kusaidia kuendeleza sekta ya nishati hususan utafutaji wa gesi asilia.

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt Hussein Mwinyi akiongea na baadhi ya wajumbe wa mkutano wa kimataifa wa Uzazi wa Mpango katika ukumbi wa Queen Elizabeth II jijini London Julai 11, 2012. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Uzazi na Malezi Bora Tanzania (UMATI), Bi Josephine Mwankusye na kulia ni Naibu Mkurugenzi wa Afya ya Mzazi na Mtoto katika Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt Neema Rusibamayila

No comments:

Post a Comment