Rais mstaafu wa awamu ya pili, Alhaji Ali Hassan Mwinyi akihutubia katika hafla hiyo ya utoaji tuzo za wanamichezo bora wa mwaka 2011.
Mzee Ali Hassan Mwinyi akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa zamani wa timu ya taifa iliyofanikiwa kushiriki mashindano ya kombe la mataifa huru ya Afrika mwaka 1980 mara baada ya kuwakabidhi tuzo ya heshima ukumbini Diamond Jubillee, Dar es Salaam, jana. Rais mstaafu wa awamu ya pili, Alhaji Ali Hassan Mwinyi akimkabidhi mchezaji wa Simba na Taifa Stars, Shomari Kapombe tuzo ya mshindi za jumla wa mwanamichezo bora wa mwaka 2011, sanjari na pesa tasli Sh milioni 12.
Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji Zanzibar(ZBC),Omar Said Ameir akikabidhi tuzo ya mchezaji bora wa Tanzania katika soka Agrey Morris anayekipiga Azam FC na Taifa Stars.Mkurugenzi wa Twanga Pepeta, Asha Baraka(kulia) akikabidhi tuzo ya bondia bora ngumi za kulipwa, Nasseb Ramadhan.
Mwenyekiti wa TASWA, Juma Pinto akimkabidhi mchezaji bora wa netiboli, Lilian Sylidion katika hafla hiyo
Mkurugenzi wa City Sports Lounge Benny Kisaka(kushoto) wakifurahia jambo na Ridhiwan Kikwete katika meza yao, Diamond Jubilee, jana.
Wadau wa mchezo wa ngumi wakiwa na mdhamini wa Kitwe General Traders, Lucas Rutta(katikati)
No comments:
Post a Comment