Friday, October 5, 2012

TIMU ZAGAWANA ELFU 6


MECHI ya ligi kuu soka Tanzania Bara kati ya African Lyon ya Dar es Salaam na Toto Africans ya Mwanza iliyochezwa kwenye Uwanja wa Azam Complex jana,ilivunja rekodi ya mapato kiduchu baada ya kila timu kugawana sh. 6,864.3.

 

Mechi hiyo ilishuhudiwa na washabiki tisa kwa kiingilio cha sh. 3,000 na kuingiza jumla ya mapato ya Sh. 27,000( Ishirini na saba elfu). Mgawo wa mechi hiyo ulikuwa VAT sh. 4,118.6 wakati Uwanja sh. 2,288.1, gharama za mchezo sh. 2,288.1, Kamati ya Ligi sh. 2,288.1, FDF sh. 1,372.8 na Chama cha soka Dar es Salaam (DRFA) kilipata sh. 915.2.

 

 

YANGA, SIMBA WAINGIZA MIL 390/-

 

KATIKA pambano la watani wa jadi Yanga na Simba la Ligi Kuu ya Vodacom lililochezwa jana kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kumalizika kwa sare ya bao 1-1 limeingiza sh. 390,568,000.

 

Watazamaji 50,455 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo iliyochezwa usiku kwa viingilio vya sh. 5,000, sh. 7,000, sh. 10,000, sh. 15,000, sh. 20,000 na sh. 30,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 93,345,549.15 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 59,578,169.49.

 

Mgawo mwingine wa mapato hayo ni posho ya msimamizi wa kituo sh. 240,000, kamishna wa mechi sh. 250,000, waamuzi sh. 591,000, mwamuzi wa akiba (reserve referee) sh. 70,000, usafi na ulinzi wa uwanja sh. 2,350,000 na Wachina (stadium technical support) sh. 2,000,000.

 

Gharama nyingine ni Umeme sh. 750,000, maandalizi ya uwanja (pitch preparation) sh. 400,000, ulinzi wa mechi sh. 5,860,000 wakati tiketi ni sh. 7,327,000. Gharama za mchezo sh. 31,115,183.05, uwanja sh. 31,115,183.05, Kamati ya Ligi sh. 31,115,183.05, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 18,669,109.83 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 12,446,073.22.

 

No comments:

Post a Comment