Sunday, October 14, 2012

Mrembo wa Ilala atwaa taji la Top Model

 


 Magdalena Roy
 MISS Dar City Center ambaye pia alishika nafasi ya pili katika shindano la Redd’s Miss Ilala, Magdalena Roy amefanikiwa kuingia 15 Bora ya Redd’s Miss Tanzania baada ya juzi usiku kufanikiwa kutwaa taji la Top Model.

 Magdalena anakuwa mrembo wa pili kuingia katika hatua hiyo, akiungana na LucyStephano kutoka Mbulu ambaye wiki iliyopita alitwaa taji la Miss Photogenic.

 Katika shindano la Top Model lililofanyika kwenye hoteli ya Naura Spring, mjini hapa lilikuwa na upinzani mkali kutoka kwa washiriki wote wa Redd’s Miss Tanzania.

 Mbali na Magdalena warembo wengine waliofanikiwa kuingia katika tano bora walikuwa ni Mary Chizi (Ilala), Irene Veda (Lindi), Belinda Mbogo (Dodoma) na Sina Revocatus (Elimu ya Juu).

 Warembo hao waliondoka jana mjini Arusha kuelekea Tanga kwa ajili ya kutembelea mapango ya Amboni, kabla ya kurejea Dar es Salaam keshokutwa.

 

No comments:

Post a Comment