Monday, August 13, 2012

Sailing Boat - Mercedes Benz Cup 2012

  Meneja Masoko wa CFAO Motors Tharaia Ahmed (Kulia) na  Mkurugenzi wa Biashara  wa CFAO Motors Wayne Mcintosh (kushoto) katika picha ya pamoja ya washindi wa kwanza hadi wa tatu walioshiriki mashindano ya Boti zinazokwenda kwa upepo (Sailing Boat) ya  Mercedes Cup 2012 baada ya kukabidhiwa vikombe na zawadi zao yaliyofanyika katika fukwe za Yatch Club jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.  Mashindano hayo yanayofanyika kila mwaka yamedhaminiwa na Kampuni ya CFAO Motors.
Meneja Masoko wa CFAO Motors Tharaia Ahmed akikabidhi Kombe kwa timu ya washindi wa  kwanza wa mashindano ya Boti zinazokwenda kwa kutumia upepo (Sailing Boat) ya Mercedes Cup 2012 Al Bush na Jeppe yaliyofanyika katika fukwe za Yatch Club Jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Biashara  wa CFAO Motors Wayne Mcintosh. Mashindano hayo yanayofanyika kila mwaka yamedhaminiwa na Kampuni ya CFAO Motors.

No comments:

Post a Comment