Tuesday, July 31, 2012

TAJIRIKA NA JAMBO LEO

Kampuni ya Jambo Concepts inayochapisha magazeti ya Jambo Leo, Staa Spoti na jarida la kila mwezi la jambo Brand Tanzania, kwa kushirikiana. a TSN Supermarket wameandaa bahati nasibu (promotion) ambayo itaendeshwa kwa muda wa miezi mitatu ikishirikisha wasomaji walio zaidi ya miaka 18.

Akizungumza na Waandishi wa Habari katika mgahawa wa City Sports Lounge, Mkurugenzi wa Jamboleo Bw. Benny Kisaka amesema msomaji wa gazeti hiloatatakiwa kukata kuponi itakayokuwa inapatikana ukurasa wa pili wa gazeti na kukusanya kuponi za matoleo saba mfululizo.
Mshindi wa kwanza katika bahati Nasibu hiyo atapata Bajaaj yenye thamani ya shilingi milioni 5,500,000/=, mshindi wa Pili atapata Sofa Set yenye thamani ya shilingi milioni 2,000,000/= huku Mshindi wa tatu akijinyakulia TV Flat Screen ya Inchi 32 yenye thamani ya shilingi 850,000/= wakati mshindi wa Nne ataambulia jokofu(fridge) yenye thamani ya shilingi 650,000/.
Gazeti hilo linaloandika habari za siasa, uchumi, jamii, burudani na michezo lilianza kutoka June 4 mwaka 2009, kila siku ambapo mwezi mmoja uliopita walianzisha gazeti jingine la linaloandika habari za michezo na burudani pekee, likiwa linatoka mara moja kwa wiki siku za Jumapili

 Mkurugenzi wa Gazeti la Jamboleo Bw. Ben Kisaka (wa pili kulia) akizungumzia project mpya ya Jambo Concept ambapo amesema katika kufurahia mafanikio ya miaka 3 na nusu ya kushiriki kikamilifu katika Tasnia hii ya habari wameamua kuandaa utaratibu wa kusheherekea na kufurahia pamoja kwa kuwashirikisha na kuwanufaisha wasomaji wa gazeti hilo linalotoka kila siku. Wa kwanza kushoto ni Afisa Masoko wa TSN Roselyn Benny, Meneja Mkuu wa TSN Group Bw. Emmanuel Ngallah na Kulia ni Meneja Mkuu Jambo Concepts Bw. Ramadhani Kibanike.

Meneja Mkuu wa TSN Group Bw. Emmanuel Ngallah (katikati) akifafanua Promosheni ya tajirika na jambo ambayo itaanza tarehe 1 Agosti mwaka huu ambapo amesema droo zao zitakuwa zikichezeshwa mara mbili kila mwezi. Kushoto ni Afisa Masoko wa TSN Roselyn Benny na Kulia ni Mkurugenzi wa Gazeti la Jamboleo Bw. Ben Kisaka.


No comments:

Post a Comment