Sunday, July 1, 2012

RAIS KIKWETE AKUTANA NA WATENDAJI WAKUU WA MAKAMPUNI MBALIMBALI YA KIMAREKANI WANAOTEMBELEA TANZANIA

Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Kimarekani na waalimu wao pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe John Haule, Balozi wa Marekani nchini, Mhe na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe Mwanaidi Sinare Maajar. Wanafunzi hao wanachukua masomo ya lugha ya Kiswahili katika Chuo Kikuu cha Zanzibar ( SUZA). Walikuwa wameongozana na Watendaji Wakuu wa Makampuni mbalimbali kutoka Marekani walipomtembelea Rais Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam Juni 30, 2012 katika ziara yao ya siku kadhaa ya kuvumbua tanzania (Discover Tanzania VIP CEOs tour iliyoandaliwa na ubalozi wa Tanzania Marekani


Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja na Watendaji Wakuu wa Makampuni mbalimbali kutoka Marekani walipomtembelea Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 30, 2012 katika ziara yao ya siku kadhaa ya kuvumbua tanzania (Discover Tanzania VIP CEOs tour) iliyoandaliwa na ubalozi wa Tanzania Marekani. Hii ni mara ya pili kufanyika ziara kama hii, ambapo pamoja na kuwakaribisha tena Rais Kikwete alisema amefurahishwa sana kwa wageni hao kuchagua kutembelea hifadhi za wanyama za kusini mwa nchi (Selous na Ruaha) vyenye wanyama wengi na vivutio ambavyo havipatikani kwingine kokote kama vile makundi ya mbwa mwitu ambayo kwa muda mrefu sasa yametoweka mbuga za Kaskazini.

No comments:

Post a Comment