Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) linatoa pongezi kwa uongozi mpya wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa
wa Dodoma (DOREFA) uliochaguliwa katika uchaguzi uliofanyika juzi (Julai 21
mwaka huu).
Ushindi waliopata viongozi
waliochaguliwa kuongoza chama hicho unaonesha jinsi wajumbe wa Mkutano Mkuu wa
DOREFA walivyo na imani kubwa kwao katika kusimamia mchezo huo mkoani Dodoma.
TFF inaahidi kuendeleza
ushirikiano wake kwa Kamati ya Utendaji ya DOREFA chini ya uenyekiti wa Nasoro
Kipenzi ambaye amechaguliwa kwa kipindi cha pili mfululizo.
Uongozi huo mpya una
changamoto nyingi, kubwa ikiwa ni kuhakikisha unaendesha shughuli za mpira wa
miguu mkoani Dodoma kwa kuzingatia katiba ya DOREFA pamoja na vyombo vya mpira
wa miguu vilivyo juu yake.
Pia tunatoa pongezi kwa
Kamati ya Uchaguzi ya DOREFA na Kamati ya Uchaguzi ya TFF kwa kuhakikisha
uchaguzi huo unaendeshwa kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi za wanachama wa
TFF.
Viongozi waliochaguliwa
katika uchaguzi huo uliofanyika hoteli ya Dear Mama ni Nassoro Kipenzi
(Mwenyekiti), Thadeo Kaliza (Makamu Mwenyekiti), Stewart Masima (Katibu Mkuu),
Kepha Maswaga (Mhazini), Mulamu Ngh’ambi (Mjumbe wa Mkutano Mkuu TFF), Mohamed
Aden (Mwakilishi wa Klabu TFF), Zawdi Kassim (Mjumbe Kamati ya Utendaji).
RAMBIRAMBI MSIBA WA
MTANGAZAJI JOSEPH MAPUNDA
Shrikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko kifo cha mtangazaji wa michezo wa Radio
Wapo, Joseph Mapunda kilichotokea juzi asubuhi (Julai 21 mwaka huu) jijini Dar
es Salaam.
Msiba huo ni mkubwa katika
sekta ya habari na mpira wa miguu kwani kwa nyakati tofauti Mapunda alifanya
kazi na TFF kwa kuripoti shughuli zetu nyingi za mpira wa miguu, hivyo mchango
wake tutaukumbuka daima.
TFF inatoa pole kwa familia ya marehemu
Mapunda, Radio Wapo na Chama cha Waandishi wa Habari Tanzania (TASWA) na
kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo
mzito.
Mungu aiweke roho ya marehemu
Mapunda mahali pema peponi. Amina
No comments:
Post a Comment