KAMATI ya uchaguzi ya chama cha soka mkoa Dar es
Salaam, DRFA leo kimetangaza utaratibu wa uchaguzi wa chama hicho unaotarajiwa
kufanyika Oktoba 14 mwaka huu, baada ya kusimamishwa shirikisho la mpira wa
miguu nchini TFF, kutokana na kasoro zilizokuwemo katika katiba yao.
Kamati imeamua kutangaza mapema fursa za wanaotaka
kuwania uongozi ndani ya DRFA mapema kabla ya tarehe 3 tuliyopanga awali, ili
kutoa wigo mpana zaidi ya wagombea. Septemba 10 itakuwa ni siku ambayo kamati ya
uchaguzi itakaa na kuzipitia fomu zote na kuweka wazi kwenye mbao za matangazo
majina ya waombaji uongozi DRFA.
Septemba 16 kutoa fursa ya pingamizi kwa waombaji
uongozi. Mwisho wa kupokea pingamizi ni Septemba 20 saa 10 alasiri. Pingamizi
ziwasilishwe kwa katibu wa kamati ya uchaguzi.
Hakutakuwa na ada katika kuweka pingamizi, bali
pingamizi zizingatie matakwa ya ibara ya 11(2) ya kanuni za uchaguzi.
Ratiba hii inaonesha Septemba 26 ni fursa ya kukata
rufaa iwapo maamuzi yaliyotolewa na kamati DRFA hayakurishishwa na mrufaa na
hiyo itakwenda kwa kamati ya TFF.
Kampeni kwa wagombea zitaanza rasmi Oktoba 4, hadi13
ambapo Oktoba 14 itakuwa uchaguzi. Pia
katika kikao cha kamati ya uchaguzi ya DRFA kilichoketi Septemba 1, imetoa ufafanuzi kuhusu waliochukua fomu awali kuwa watachukua
tena, lakini hawatalipa ada ya kuchukua fomu.
Ada kwa nafasi ya Mwenyekiti, Makamu na Katibu ni
Sh. 200,000 wakati nafasi nyingine zote ni Sh.100,000 na kuwa kipengele pekee
kilichotakiwa marekebisho cha kiwango cha elimu kimerekebishwa na hakuna sehemu
inayosema inayofanana na, bali elimu ya kidato cha nne.
No comments:
Post a Comment