Bendi ya Mashujaa Musica, ndiyo itakayolinogesha shindano la Redds Miss Temeke, litakalofanyika Ijumaa Sept 21, kwenye ukumbi wa PTA(Sabasaba Hall), ikiwa ni funga dimba ya mashindano ya urembo jijini Dar es Salaam na mikoani kwa ujumla kwa mwaka huu.
Mashujaa inayoundwa na wanamuziki wengi nguli akiwemo Charles Baba, MCD, Ferguson, Ali Akida na wengineo, ni mara yao ya kwanza kufanya shoo katika mashindano ya kanda, hivyo wamejipanga vilivyo kukidhi kiu ya mashabiki wao.
Mbali ya Mashujaa, msanii nguli katika kundi la Ze Comedy Original, Mpoki sanjari na Steve Nyerere watainogesha Redd's Miss Temeke, ikiwa ni buradani tosha kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam, ambao tayari wamekwisha shuhudia shoo za Redd's Miss Ilala na Redd's Kinondoni zilizofanya mwanzo.
Taji la Redd's Miss Temeke, linashikiliwa na mrembo Husna Twalib. Warembo wa Miss Temeke wamekuwa wakijifua kwa wiki tatu sasa chini ya ukufunzi wa Leyla Bhanji, ambaye amekuwa akisaidiwa pia na warembo wa miaka ya nyuma wa Miss Temeke akiwemo, Regina Mosha(20020, Hawa Ismail(2003), washiriki wa mwaka jana Joyce Maweda, Mwajabu Juma, Cynthia Kimasha na katika shoo wamekuwa na Dickson Daud kutoka kundi la THT.
Shoo ya ufunguzi itakuwa tofauti kabisa na shoo nyingine yeyote iliyowahi kuyanyika nchini, kwani imezingatia zaidi urembo na nini msichana anatakiwa kufanya na si unenguaji tu. Warembo 15 wanatoka katika vitongoji vya Kigamboni, Kurasini na Chang'ombe ambapo kila sehemu wametoka warembo watano ambapo washindi watatu wa kwanza watapata fursa ya moja kwa moja kushiriki Redds Miss Tanzania 2012.
Warembo hao ni Agness Goodluck, Angela Gasper, Flaviana Maeda,Edna Sylvester, Catherine Masumbigana, Khadija Kombo, Neema Doreen, Flora Kazungu, Lilian Joseph, Elizabeth Peter, Elizabeth Boniphace, Jesca Haule, Zulfa Bundala, Mariam Ntakisivya na Esther Albert.
Temeke imewahi kutwaa taji la Miss Tanzania mara tatu, kupitia warembo Happiness Sosthenes Magesse aka Millen mwaka 2001, Sylvia Remmy Baham mwaka 2003 na Genevieve Mpangala.
Lakini pia imetoa warembo waliowahi kushika nafasi ya pili na tano bora katika Miss Tanzania kama Jokate Mwegelo, Irene Uwoya, Irene Kiwia, Queen David, Cecylia Assey, Sabrina Slim, Miriam Odemba, Ediltruda Kalikawe na Asela Magaka.
Mbali ya Redd's, Miss Temeke 2012 pia imedhaminiwa na Kampuni ya GlobalPublishers kupitia magazeti yake pendwa na Website yao, Dodoma Wine, gazeti la Jambo Leo, Push Mobile, City Sports Lounge, Mariedo Boutique, 100.5 Times FM, Kitwe General Traders, Fredito Entertainment, katejoshy.blogsport.com na 88.4 Cloud's FM.
No comments:
Post a Comment