Amesema hayo leo, wakati akiongea
na mwandishi wa habari ofisini kwake aliyetaka kujua fursa za ajira zilizoko na
taratibu za mchakato wa ajira tangu kutolewa kwa tangazo hadi kupangiwa kituo
cha kazi.
Daudi amesema, kwa mfano
mwananchi yeyote akitembelea katika tovuti ya Sekretarieti ya Ajira hivi sasa
ataona tangazo la kuitwa kazini kwa waombaji kazi waliofaulu katika usaili
uliofanyika mwezi Juni, 2012 ambao wanatakiwa kuripoti kwa Waajiri; Wakala wa
Vipimo, pamoja na kwa Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii.
Mbali na hilo, pia watakuta
tangazo la kuitwa kwenye usaili kwa wale waliokidhi vigezo kulingana na nafasi
walizokuwa wameomba kama zilivyokuwa zimetangazwa kwa niaba ya Halmashauri ya Wilaya
ya Babati, Chuo cha Mipango Dodoma, Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo,
Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo na taasisi nyinginezo.
Aliongeza kuwa katika Tovuti
hiyo watakuta pia tangazo la nafasi za kazi 194 zikiwemo nafasi za Wakurugenzi,
Wakufunzi Waandamizi wa Vyuo, Wakufunzi Wasaidizi, Wahandisi, Mafundi Sanifu, Wakaguzi
wa ndani wa hesabu, Makatibu Mahsusi, Walinzi, Wapishi na kada nyinginezo.
Aidha, amesisitiza ni muhimu
kwa waombaji kuzingatia masharti ya tangazo pindi wanapotuma maombi yao kwa
njia ya posta ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kupata fursa ya ajira
serikalini maana mchakato wa ajira hufuata Sera, Sheria, Kanuni na Taratibu
Katibu wa Sekretarieti ya
Ajira alimaliza mahojiano yake kwa kuitaja tovuti ya Sekretarieti ya Ajira kuwa
ni www.ajira.go.tz kwa wale wasioifahamu ili
waweze kuifahamu.
No comments:
Post a Comment