Klabu tano za Ligi Kuu ya
Tanzania zimewasilisha Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) majina ya
wachezaji ambao zimewakatishia mikataba/mikataba yao kumalizika au kuwaacha kwa
ajili ya usajili wa wachezaji msimu wa 2012/2013.
Kwa mujibu wa klabu hizo,
Polisi Morogoro iliyopanda msimu huu imeacha wachezaji 17 wakati Tanzania
Prisons ambayo pia imepata hadhi ya Ligi Msimu huu imeacha wachezaji 11. Azam
imekatisha mikataba ya wachezaji watatu.
Wachezaji 12 wamemaliza
mikataba yao katika klabu ya Kagera Sugar wakati wakati kwa upande wa Simba
wachezaji waliomaliza mikataba ni wanne huku ikionesha nia ya kuwatoa kwa mkopo
wengine wanne.
Uhamisho wa wachezaji kwa
msimu huu ulianza Juni 15 mwaka huu na utamalizika Julai 30 mwaka huu wakati
kipindi cha kuanza wachezaji (kwa wasio wa Ligi Kuu) ni kati ya Juni 15 na 30
mwaka huu.
Kwa klabu za Ligi Kuu
kutangaza wachezaji watakaositishiwa mikataba yao ni kuanzia Juni 15-30 mwaka
huu na usajili wa wachezaji unafanyika kuanzia Juni 15 hadi Agosti 10 mwaka
huu.
Wachezaji walioachwa Polisi
Morogoro ni Abdul Ibadi, Ally Moshi, Benedict Kitangita, Hassan Kodo, Hussein
Lutaweangu, Hussein Sheikh, Juma Maboga, Mafwimbo Lutty, Makungu Slim, Mbaraka
Masenga, Method Andrew, Moses Mtitu, Ramadhan Kilumbanga, Ramadhan Toyoyo, Said
Kawambwa, Salum Juma na Thobias John.
Tanzania Prisons imewaacha
Adam Mtumwa, Dickson Oswald, Exavery Mapunda, Ismail Selemani, Lwitiko Joseph,
Mbega Daffa, Mwamba Mkumbwa, Musa Kidodo, Rajab Ally, Richard Mwakalinga na
Sweetbert Ajiro.
Wachezaji waliomaliza
mikataba yao kwa mujibu wa Kagera Sugar ni Cassian Ponera, Hamis Msafiri,
Hussein Swedi, Ibrahim Mamba, Martin Muganyizi, Mike Katende, Moses Musome,
Msafiri Davo, Said Ahmed, Said Dilunga, Steven Mazanda na Yona Ndabila.
Azam imewasitishia mikataba
wachezaji Tumba Swedi, Mau Bofu na Sino Augustino. Wachezaji waliomaliza
mikataba Simba kwa mujibu wa klabu hiyo ni Ally Mustafa, Derick Walulya, Gervais
Kago, Juma Jabu wakati Salum Kanoni mkataba wake unatarajia kumalizika Juni 30
mwaka huu.
Wachezaji ambao Simba
inakusudia kuwatoa kwa mkopo ni Rajab Isihaka, Salum Machaku, Haruna Shamte na
Shija Mkina.
DODOMA YAITAMBIA MBEYA COPA
COCA-COLA 2012
Dodoma imeendeleza wimbi la
ushindi kwenye michuano ya Copa Coca-Cola 2012 baada ya leo asubuhi (Juni 27
mwaka huu) kuifunga Mbeya mabao 2-0 katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Tamco
ulioko Kibaha mkoani Pwani.
Mabao ya Dodoma katika mechi
hiyo ya kundi C yalifungwa na Japhet Lunyungu dakika ya 59 wakati Frank Kaji
aliwahakikishia ushindi washindi dakika saba kabla ya filimbi ya mwisho baada ya
kupachika bao la pili.
Nayo Mjini Magharibi
iliifunga Iringa mabao 3-0 katika mechi ya kundi B iliyochezwa leo asubuhi
kwenye Uwanja wa Nyumbu mkoani Pwani.
Mechi za asubuhi zilizokuwa zichezwe leo kati
ya Arusha na Kusini Pemba kwenye Uwanja wa Tanganyika Packers na Pwani na Tabora
kwenye Uwanja wa Karume sasa zitachezwa kuanzia saa 8 mchana kutokana na
kutokuwepo mawasiliano ya barabara asubuhi (Morogoro Road) kutoka mkoani Pwani
kuingia Dar es Salaam.
Leo jioni kutakuwa na mechi
kati ya Rukwa na Ruvuma (Tanganyika Packers), Mwanza na Tanga (Nyumbu),
Kaskazini Unguja na Mara (Tamco) na Singida na Kagera (Karume).
No comments:
Post a Comment