Monday, September 17, 2012

KAMATI YA MISS TZ


Kamati ya Miss Tanzania leo inatarajiwa kutembelea kambi ya Redd’s Temeke 2012, kubwa ni kuwafunda vimwana hao kutoka Vitongoji vya Kigamboni, Kurasini na Chang’ombe, kuhusu mambo mbalimbali ndani ya mashindano ya urembo.
Kamati hiyo itaongozwa na Mkurugenzi wake, Hashim Lundenga atakayefuatana na mshauri wa masuala ya urembo katika kamati yao, Dk. Ramesh Shah, katibu Bosco Majaliwa, Mkuu wa Itifaki, Albert Makoye na mjumbe wa kamati hiyo, Lucas Rutta.

Shindano la Redd’s Miss Temeke, linafanyika Ijumaa hii katika ukumbi wa PTA(SabaSaba Hall) na tiketi za VIP zimeshaanza kuuzwa katika Club za City Sports Lounge iliyopo makutano ya Samora na Azikiwe na Nyumbani Lounge iliyopo maeneo ya Namanga ambapo VIP kwa mtu mmoja ni Tshs 50,000 na pia waweza nunua kwa meza moja ama ya watu 8 kwa laki 4 au watu kumi laki 5.
Warembo hao ni Agness Goodluck, Angela Gasper, Flaviana Maeda,Edna Sylvester, Catherine Masumbigana, Khadija Kombo, Neema Doreen, Flora Kazungu, Lilian Joseph, Elizabeth Peter, Elizabeth Boniphace, Jesca Haule, Zulfa Bundala, Mariam Ntakisivya na Esther Albert.

Mbali ya vinywaji vya Redd’s  na Dodoma Wine, Miss Temeke pia imedhaminiwa na gazeti la Jambo Leo, katejoshy.blogspot.com, Mariedo Boutique, Push Mobile, City Sports Lounge, 100.5 Times FM, Kitwe General Traders, Global Publishers na 88.4 Cloud’s FM.
  Warembo wanaowania taji la Redd’s litakalofanyika Ijumaa hii Sept 21, kwenye ukumbi wa PTA(Sabasaba Hall), wakiwasiliza wakufunzi wao kutoka kulia Joyce Maweda, Leyla Bhanji, Hawa Ismail na Mwajabu Juma wakati wa mazoezi yao jana kwenye Club ya TCC Chang’ombe.(Picha BMP Promotions)

Warembo wanaowania taji la Redd’s wakiwa mazoezini jana kwenye Club ya TCC Chang’ombe jana. Shindano hilo litafanyika Ijumaa hii Sept 21, kwenye ukumbi wa PTA(Sabasaba Hall).(Picha na BMP Promotions)

No comments:

Post a Comment