Kim K
Friday, August 3, 2012
RAIS KIKWETE ATOA KIFUTA JASHO CHA NG'OMBE KWA WANANCHI WA MONDULI
SERIKALI itakuwa inagawa ng’ombe 1500 kila mwezi kwa wananchi wa wilaya tatu za Mkoa wa Arusha kama kifuta jasho cha kupoteza kiasi cha karibu mifugo 800,000 iliyopotea kutokana na ukame na athari zake mwaka 2008/2009.Ahadi hiyo imetolewa leo, Alhamisi, Agosti 2, 2012 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete wakati alipozindua Mradi wa Serikali wa Uwezeshaji Mifugo kwa waliopotelewa mifugo yote katika Wilaya ya Monduli kwenye sherehe iliyofanyika Makuyuni wilayani humo.
Katika uzinduzi huo uliohudhuriwa na viongozi wa Mkoa wa Arusha wakiwemo wakuu wa wilaya na wabunge wa mkoa huo, Rais Kikwete amegawa ng’ombe 500 kwa kundi la kwanza la wananchi ikiwa ni mitamba minne na dume moja la kisasa kwa kaya 16 za mwanzo.
Uzinduzi huo ni wa pili kufanywa na Rais Kikwete chini ya Mradi huo wa kwanza wa aina yake kubuniwa na Serikali katika historia na wenye thamani ya sh. Bilioni 12.9.
Februari 19, mwaka huu, Rais Kikwete alizindua Mradi kama huo katika Wilaya ya Loliondo kwenye sherehe zilizofanyika mjini Loliondo. Kesho Agosti 3, 2012 Rais Kikwete anatarajiwa kuendelea na zoezi hilo katika mji wa Loliondo
JK MONDULI
Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Wananchi wa kijiji cha Makuyuni,Wilayani Monduli leo wakati alipofika kuzindua mpango wa kugawa ng'ombe 1500 kila mwezi kwa wananchi wa wilaya tatu za Mkoa wa Arusha kama kifuta jasho cha kupoteza kiasi cha mifugo 800,000 kutokana na ukame na athari zake mwaka 2008/2009.
Rais Jakaya Kikwete akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Makuyuni,Wilayani Monduli mchana wa leo wakati alipofika kuzindua mpango wa kugawa ng'ombe 1500 kila mwezi kwa wananchi wa wilaya tatu za Mkoa wa Arusha kama kifuta jasho cha kupoteza kiasi cha mifugo 800,000 kutokana na ukame na athari zake mwaka 2008/2009.
Rais Jakaya Kikwete akimkabidhi ng'ombe mmoja wa wakaazi wa Monduli walioathririka na ukame mwaka 2008/2009 ambapo walipoteza mifugo yao yote. Hafla hii imefanyika leo katika kijiji cha Makuyuni,Wilayani Monduli.
Thursday, August 2, 2012
Wednesday, August 1, 2012
OFFICIAL VIDEO-LEKA DUTIGITE VIDEO-KIGOMA ALL STARS
Kigoma All Stars-Leka Dutigite -Abdu kiba, Baba Levo, Banana Zorro, Chege, Diamond plantimuz, kigoma all stars, Leka Dutigite, Linex, Makomando, Mwasiti, Ommy dimpoz, Queen Darling,Rachel, Zitto Kabwe.
In this Video the beuty of kigoma is well seen i love the water fall and everything in this video, bigup to all Kigoma All Stars mmetokelezea!!!!!!!!!!1
Subscribe to:
Posts (Atom)
























